HATIMAYE, mrembo Georgina Njenga amemtambulisha
mpenzi mpya, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya uhusiano wake wa awali
kusambaratika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Georgina Njenga alichapisha msururu wa picha akiwa na mpenzi mpya.
Mama huyo wa mtoto mmoja, binti, alifuatisha picha hizo na ujumbe wa kimahaba akimtaja kijana huyo mwenye habati kama mfalme wa himaya ya moyo wake. Akionesha ukaribu wao ulivyokolea, Njenga aliweka wazi kwamba kumbukumbu nzuri ya mwaka huu kwake ni kumpata yeye.
“Hey mpenzi wangu, kumbukumbu pendwa kwangu mwaka huu imekuwa kukutana na wewe. Wewe ndiye kitu kizuri kuwahi kutokea kwangu na kusema kweli hatimaye kusema nina mtu wa kupenda ni hatua kubwa nwangu,” Georgina Njenga alisema.
“Nakupenda sana mpenzi wangu na shukrani kwa kunielewa kwa kina ambacho hakuna yeyote amewahi kuelewa. Kwa kweli, wewe umetumwa kutoka kwa Mungu mpenzi wangu,” Georgina aliongeza.
Mwaka jana mwezi Julai, Georgina Njenga na baba binti yake, Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari walitangaza kuachana baada ya penzi lao kudumu kwa miaka michache.
Kuachana kwao kulijiri wiki chache baada ya Baha kudaiwa kuingia katika uraibu wa Kamari za mitandaoni.
Hata hivyo, Georgina Njenga mwezi Februari mwaka huu katika mahojiano, alifunguka kwa kina akielezea kiini cha penzi lao kuvunjika.
Akiongea kwenye mahojiano na SPM Buzz, Georgina alifichua kuwa sababu kubwa iliyomfanya aachane na Tyler ni kwa sababu wote wawili walikuwa na malengo tofauti, jambo lililowafanya waone ni bora waachane, na kuongeza kuwa uhusiano wao haukuwa na mafanikio hata kidogo.
“Katika mahusiano, maeneo ya Inafika, kila mmoja wenu ana malengo tofauti… nilikuwa na malengo tofauti; alikuwa na malengo tofauti, na hatukuweza kufikia malengo yetu kwa njia moja ...Mambo mengi ya kibinafsi hayakuwa yakifanya kazi, ambayo nisingependa kuyazungumzia hapa,” Georgina alishiriki.
Mama wa mtoto mmoja alishiriki zaidi maoni yake juu ya kuokoa uhusiano akikushauri zaidi ikiwa umejaribu kuongea na bado haifanyi kazi, ni sawa sana kuondoka, kwani huna haki.
"Binafsi, siamini kila kitu kinapaswa kuwa milele. Ikiwa haifanyi kazi na ninyi mmejaribu, mnaweza kuiacha iende, "Georgina alishiriki.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!