Msanii wa Mugithi, Samidoh ameumwaga moyo wake wa shukrani kwa mashabiki wake baada ya kuufanya wimbo wake mpya kushikilia kidedea katika nyimbo maarufu kwenye YouTube.


Samidoh aliachia wimbo wake mpya wa Wendo wa Ihera takribani wiki moja iliyopita, na licha ya kuimba kwa lugha ya Agikuyu, wimbo huo umeibuka kuwa pendwa miongoni mwa Wakenya wa matabaka mbalimbali.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wimbo huo unazungumzia mapenzi ya sumu kutoka kwa mpenzi mwenye hulka mbaya na ndani ya siku tano tu, tayari umetazamwa zaidi ya mara milioni moja kwenye jukwaa la YouTube.


Samidoh alichukua kwenye kurasa zake katika mitandao ya kijamii akishukuru mashabiki kwa kumfikisha hapo, akisema kwamba hiyo ni rekodi mpya katika kariha yake ya muziki.


Alisema pia kuwa kando na wimbo kutazamwa mara milioni moja, ulimvutia mashabiki wengi na tayari amefikisha mashabiki waliojisajili kwa chaneli yake hadi nusu milioni.


“Mashabiki wapendwa, Huenda nisiweze kamwe kukushukuru ya kutosha kwa jinsi unavyoniunga mkono, kila wakati mwingine. Wakati huu nikiwa na WENDO WA IHERA~Mapenzi ya Sumu, nilijihatarisha na kuamua kujaribu kitu nje ya eneo langu la faraja, Kusema kweli Mapokezi yako yameniacha nikiwa nimeshangaa, kunyenyekea na kunitia moyo.”


“Utazamaji wa MILIONI 1 kwenye Youtube ndani ya Siku 5!!ni REKODI MPYA kwangu na bonasi ya mashabiki zaidi ya 500k ili kuiongeza na bado inavuma kwa nambari 1 !!Huyu anaweza kuwa Mungu pekee!! Mifuko yako Isikauke Kamwe na Mungu akutane na wewe kila wakati kwenye hitaji lako,” Samidoh aliandika.