Mwanamke mmoja amekuwa gumzo la mtandaoni baada ya
kuandika ujumbe mrefu wa shukrani kwa mume wake.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, aliandika ujumbe wa
kumshukuru mume wake kwa kuwa na moyo wa kumsamehe baada ya kutoka nje ya ndoa
yao na hata kupata mtoto na mwanamume mwingine.
Alisema kwamba aliwahi kumsaliti mpenzi wake na zao la kitendo hicho likawa ni mwanaharamu lakini bado mume wake alimsamehe na kumrudisha kwa ndoa yao.
“Nilipokusaliti, ULIBAKI! Nilipokuwa na mtoto nje ya ndoa, ulinitunza! Nilipokuacha ukiwa chini kabisa, ULINIrudisha ulipokuja!” sehemu ya ujumbe wake ilisomeka.
Mwanamke huyo alifunguka zaidi kwambahata kwa wakati mmoja aliamua kutoroka ndoa yake na kuolewa na jamaa mwingine lakini bado mambo yalipokwenda upogo katika ndoa hiyo, mume wake wa kwanza ambaye ako naye hadi sasa alifungua mikono yake na kumkaribisha.
“Nilipoolewa na kukuambia kuwa bado tunaweza kuchumbiana faraghani, ULIKUBALI!”
“Baby, siku uliyoniambia heri uwe na mimi kuliko kutokuwa na mimi kabisa, ulinifanya nitambue mapenzi yasiyo na masharti ni nini. Umenipenda kwa dhati na kwa yote niliyokuweka, bado unanichagua. Wewe ndiye ufafanuzi wa kweli wa mfalme! Napenda jinsi unavyonipenda!” alimaliza.
Chapisho hilo lilisambaa kwa kasi, huku watu wengi wakimkosoa Minnie kwa kukiri hadharani tabia ambazo baadhi yao waliziona kuwa zisizo na heshima na za kinyonyaji.
Wakosoaji walimtaja mpenzi wake kama "mlango" wa kuvumilia unyanyasaji kama huo, huku wengine wakisema kwamba matendo yake hayana heshima na uwajibikaji.
Katika video iliyofuata, Minnie alizungumzia hali hiyo, akimtetea mpenzi wake na kulaani wale wanaomkosoa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!