MKE wa Marioo, Paula Kajala amechukua kwenye mitandao ya kijamii kulalamika jinsi picha yake ilivyotokea wakati anahudhuria hafla ya mtangazaji wa Wasafi FM, Juma Lokole.


Lokole alichapisa picha hiyo akiwa na Paula ikimuonesha mrembo huyo mama wa mtoto mmoja akiwa na muonekano usio wa kawaida kwa mashabiki wake.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Paula alitokea akiwa amevaa nguo kubwa refu iliyokaa kama inamvaa na kuficha kabisa umbo lake zuri, jambo lililowafanya mashabiki wake kuduwaa.


Paula alielekea kwenye picha hiyo katika ukurasa wa Juma Lokole na kuweka wazi hisia zake za mafadhaiko, akisema ajapenda jinsi mpiga picha alivyoitoa picha yake.


Kwa mujibu wa Paula Kajala, mpiga picha aliificha, au kuififisha shepu lake na kumfanya kuonekana kama mama tu aliyepotelea ndani ya dera.


Mpiga picha kapeleka wapi shepu yangu sijapenda???,” Paula Kajala alimaka.


Paula ameolewa mwaka mmoja tu uliopita kwa msanii Marioo na tayari wana mtoto mmoja.


Katika mahojiano ya hivi majuzi, mrembo huyo wa muigizaji mkongwe wa filamu za Uswahilini, Fridah Kajala Masanja alisema kwamba angependa sana kama mpenzi wake angeirasmisha ndoa yao kabisa kwa harusi.


Alipoulizwa ni kipi anachokipa kipaumbele kati ya kurudi shuleni kumalizia masomo na kufunga ndoa, Binti Kajala alisema bila kuwaza mara mbili mbili kwamba angechagua ndoa kwanza, masomo baadae.


“Nitaendelea na masomo, nasubiri Amarah akue kwanza. Hiyo inawezekana. Mimi nataka niendelee kusomea fasheni kwa sababu ndicho kitu ambacho nakipenda. Ninataka kujiendeleza kwenye hilo,” Paula Kajala alisema.

“Hata hivyo bado mipango ya ndoa naitaka sana. Nataka kuolewa kwanza masomo baadae,” aliongeza.

Marioo alipoulizwa kuhusu hoja hiyo ya mpenzi wake, alikiri kwamba ni suala la muda tu kwani sehemu kubwa wameshaifanya tayari ikiwa ni pamoja na kuonana na kujuana na wakwe, katika shughuli ya kutambulisha jinsia ya mtoto wao miezi michache kabla ya kuzaliwa kwake.

“Suala na ndoa ni jambo jema, na sisi tumeshakuwa familia. Katika vitu vilivyotokea hapa, ina maana suala la ndoa ni suala dogo sana. Ni suala tu la kuamua, na sheria tuwe tushaifuata maana vitu vingi vya msingi tumeshavifanya kwa hiyo imebakia tu sisi kusema kwamba jamani tarehe Fulani tunataka tuoane, tufunge pingu za maisha,” Marioo alikariri kauli ya mpenziwe.

“Nitamuoa kwa sababu mwanzo nampenda, pili amenizalia binti mzuri na naheshimu uamuzi wake. Kwa hivyo, kama hitaji lake ni ndoa tu hilo ni suala dogo na limeisha,” Marioo aliongeza.