KLABU ya Shabana FC
inayoshiriki ligi kuu ya humu ncini, FKFP-PL imetangaza maokoto kutoka kwa
mechi yao dhidi ya KCB wikendi iliyopita.
Mechi hiyo ya mzunguko wa 14 ya FKFP-PL ilichezewa katika uga wa Gusii ambao ni wa nyumbani kwa Shabana ambapo walipata ushindi wa 2-0.
Zaidi ya ushindi huo muhimu dhidi ya wanabenki, Shabana FC pia ilikusanya hela zipatazo Ksh 1,015,000 kutoka kwa mauzo ya tiketi za kuingia uwanjani kwa mashabiki.
Klabu hiyo ilitoa taarifa hiyo kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii na kuwashukuru mashabiki wa nyumbani kwa kujitokeza kwa wingi kushabiki timu yao.
“Tulikusanya mapato ya jumla ya 1,015,000/=. Asante sana kwa wote waliofanikiwa kufika uwanja wa Gusii kwa mechi yetu dhidi ya KCB Fc. Ilikuwa nzuri kuona Uwanja umepakwa rangi nyekundu na nyeupe. ASANTE KWA UPENDO NA MSAADA,” Shabana FC ilisema.
Mchezaji Brian Michira alitikisa nyavu dakika ya 29 baada ya kurudisha shuti kali lililookolewa na Matthew Tegisi, huku Odongo, akitokea benchi kipindi cha pili, alitumia vyema ubovu wa safu ya ulinzi wa KCB na kumaliza kwenye lango la karibu, na kuututumua umati kwa mbwembwe.
Kufuatia ushindi wao dhidi ya KCB, klabu ya Shabana ilijipenyeza hadi nafasi ya 5 na pointi 20, pointi 4 tu nyuma ya viongozi KCB.
Shabana FC sasa wameenda mechi 4 mfululizo bila kupoteza kwa mara ya kwanza tangu kujiunga na ligi kuu msimu mmoja uliopita.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!