Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca amefafanua kwa kina ni kwa nini anasisitiza timu yake bado haiku katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya premia msimu huu.


Maresca anasisitiza Chelsea bado wako mbali kutoka kuwania ubingwa licha ya timu hiyo kuwa katika fomu nzuri na kushikilia nafasi ya pili kwenye jedwali.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kufuatia ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Brentford Jumapili usiku, Chelsea waliimarisha zaidi nafasi yao ya 2 na kupanda pointi 2 tu nyuma ya vinara Liverpool.


Lakini alipoulizwa kama sasa anaamini vijana wake wanaweza shindania ubingwa msimu huu, Enzo Maresca aliiambia BBC kwamba hiyo ni ndoto ya Alinacha.


Alieleza sababu za msimamo wake huo, akisisitiza kwamba bado timu ina mapungufu kiasi ambayo yatahitajika kuimarishwa kabla ya kujitosa rasmi katika kinyang’anyiro cha ubingwa wa EPL misimu ya usoni.


“Sio kuhusu ni mechi ngapi tunashinda. Ni juu ya kuwa wa kweli. Kuna vitu tunapaswa kufanya vizuri zaidi. Ndio maana nilisema kwa ajili yangu hatuko tayari,” Maresca alisema.


Muitaliano huyo aliendelea kummiminia sifa mshambuliaji wake Nicolas Jackson akisema kuwa licha ya kukosa nafasi za wazi wakati mwingine, lakini bado yeye ni mtu wa maana kwenye timu.


"Nilisema baada ya mechi ya Tottenham hakufunga lakini alifanya jambo la muhimu zaidi. Wengine walikuwa wakisherehekea na yeye pekee ndiye aliyeuchukua mpira. Nje ya mpira alifanya kazi kwa bidii."