
Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu iwapo wimbo huo ulimhusu Kasongo wa Kanema, Mkongo aliyefariki miaka miwili iliyopita na kuzikwa kwenye makaburi ya Lang'ata.
Wengine wanadai kuwa wimbo huo ulimhusu Songoley Kasongo, mwenzake Kanema katika bendi ya muziki ya Super Mazembe iliyojipatia umaarufu mkubwa nchini.
Wote wawili walicheza katika bendi hiyo maarufu ya Kongo iliyohamia Kenya mnamo 1974.
Vyanzo vya habari vinadai kuwa wanabendi wa Super Mazembe walimtembelea rafiki yao Kasongo huko Eastleigh, Nairobi.
Walipofika nyumbani kwake, walimuuliza mkewe kama alikuwa nyumbani.
Aliwafahamisha kuwa hajamwona mumewe, Kasongo, siku nyingi.
Wakati huo, hakukuwa na mtandao na ilikuwa nadra kupata mtu mwenye simu.
Kwa matumaini kwamba angesikia, waliamua kuzungumza naye kupitia muziki.
Washiriki wa Super Mazembe walianza kumwandikia Kasongo wimbo sebuleni kwake, wakimsihi arudi nyumbani kwa sababu mkewe ana wasiwasi na hawezi kumpata.
Wimbo huo umehusishwa kimakosa na Kassongo wa Kanema Jean Claude, aliyekuwa akiishi Bwombe Bwombe wakati unatungwa.
Inamhusu Songoley Kasongo, mpiga gitaa wa Super Mazembe. Dodo Doris, mpiga tumba wa bendi hiyo, alikuwa ameambatana na mtunzi Katele nyumbani kwa Songoley.
Wakati wimbo unaandikwa, Kasongo hakuwepo nyumbani. Bendi hiyo wakati huo ilikuwa na Didos Longwa Mutonkole (kiongozi wa bendi), Djili Loboko, Kasongo Songoley, Atia Jo, Dodo Doris, Bukasa wa Bukasa, Alley Katele, Kayembe Miketo Rapok, Lovy Longomba na Kasongo wa Kanema.
Wimbo
Kwaya
Kasongo ye yeee, mobali na ngai [Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo [Kasongo ninakufa]
Zonga libala ee [Rudi kwenye ndoa] x2
Kasongo yo yo, mobali na ngai [Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo [Kasongo ninakufa]
Zonga libala ee [Rudi kwenye ndoa]
Kwaya
Nga na ndako Kasongo [Nikiwa ndani ya nyumba, Kasongo]
Miso na nzela [Kukodolea macho barabarani kila wakati]
Soki okozonga dia ee [Kama utawahi kurudi]
Yebisa nga ye ee [Nijulishe mpenzi]
Kwaya
Libala na ndako Kasongo [katika aina hii ya ndoa]
Batunaka ngai [Wako busy kunihoji] Tata azali wapi ee [Baba yuko wapi]
Naloba nini ee [Ninasema nini]
Kwaya
Kasongo yo yo, mobali na ngai [Kasongo mume wangu]
Kasongo nga nawe oo [Kasongo nakufa]
Zonga libala ee [Rudi kwenye ndoa] [kwaya]
Nga na ndako Kasongo [Akiwa ndani ya nyumba Kasongo]
Miso na nzela [Kukodolea macho barabarani kila wakati]
Soki okozonga di
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!