SOSHOLAITI mwenye utata kutokea taifa la Nigeria,
Bobrisky ameibuka na utani mwingine tena akijitaja kama kitu cha thamani zaidi
ambacho kimewahi tokea katika taifa la Nigeria.
Bobrisky, mwanamume aliyebadili jinsia alidai kwa mikogo kwamba hakuna mwanamke mwenye thamani kubwa amewahi tokea Nigeria kumzidi yeye.
Alichukua kwenye instastory yake na kusema kwamba kwa sasa ameshakua zaidi ya viwango vya kujihusisha na kile wanablogu wa Nigeria wanasema juu yake.
Bobrisky alijinadi kwamba kwa sasa yeye amepaa viwango na anachezea ligi za wanasosholaiti maarufu wa kimataifa kama vile Kim Kardashian na wengine.
Maneno yake…
"Mimi ni msichana mzuri zaidi ambaye Nigeria imewahi toa kwa dunia. Sina biashara yoyote tena na blogu za Kinigeria, mimi ni wa viwango vya kimataifa.”
Kauli yake inajiri siku chache tu baada ya kuacha wengi wakiwa na minong’ono mtandaoni baada ya kufichua kuwa anaona siku zake za mwezi.
Mwanamume huyo aliyerjibadili jinsia kufuatia msururu wa upasuaji wa urembo alikiri kwamba kwa sasa anajihisi kuwa mwanamke kamili, lakini akalalamikia uchungu wa hedhi.
“Kusema kweli sasa hivi najihisi kabisa kuwa mwanamke aliyekamilika. Wakati mwingine huwa navunjika kwa kilio wakati niko kwenye siku zangu za mwezi, kwa sababu ni uchungu sana,” Bobrisky aliandika.
Kauli yake kudai kwamba amepaa viwango na kuingia kimataifa inajiri wakati ambapo amekuwa na msururu wa kesi na tume ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, EFCC.
Bobrisky anahusishwa na utakatishaji wa fedha na kudharau sarafu ya Naira, baada ya kukamatwa mwaka jana aliporekodiwa akirusha noti za Naira kwenye sakafu klabuni katika usiku wa tafrija.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!