RAPA na YouTuber Diana
Marua ni mmoja kati ya washawishi wa mitandao ya kijamii wa humu nchini ambao
wanamaliza mwaka wa 2024 kwa furaha na ari ya ajabu.
Mama huyo wa watoto watatu amefichua kwa mashabiki wake kwamba yeye hatokuwa miongoni mwa wale wanaomaliza mwaka kwa kinyonge, kwani umekuwa moja kati ya miaka yenye mafanikio ya kipekee katika maisha yake.
Zikiwa zimesalia siku 20 tu kukunja jamvi la 2024, Diana Marua ameweka wazi kwamba anamaliza mwaka kwa nguvu kwani tayari ameshajikusanyia vipande 8 vya mashamba katika Maeneo mbalimbali nchini kwa mwaka huu pekee.
Alipiga picha akiwa na hatimiliki 8 za mashamba yake, akisema kwamba lengo ni kuendelea kuongeza utajiri wake mwaka ujao, kwani hii ni mwanzo tu.
“Lengo ni kumaliza imara ?? mwaka gani! 2024, hatimiliki 8 tajiri zaidi ? ? Nimetimiza ndoto yangu ya 2024! ? Hatimaye nilipata vipande vya ardhi katika maeneo tofauti, na hebu niambie - hiyo kitu imenitoka!” Diana Marua aliandika kwa furaha ya ajabu.
Mke huyo wa msanii Bahati Kioko bila shaka ni mmoja wa wale ambao bidii yao imedhihiri wazi wazi kwa matokeo mwaka huu.
Huu ndio mwaka ambao Diana Marua na mpenziwe Bahati Kioko walikuwa wanandoa wa kwanza kufanikisha shoo yao ya kihalisia katika jukwaa kubwa la utiririshaji la Netflix.
Marua na Bahati pia waliweza kumtambulisha mtandaoni binti yao, Malaika ambaye hivi majuzi amesherehekea kutimiza umri wa miaka miwili.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!