Cross-dresser maarufu
kutoka Nigeria, Idris Okuneye maarufu kama Bobrisky amezua mjadala pevui
mitandaoni baada ya kuweka wazi malalamiko anayopitia kama mwanamke.
Bobrisky, mwanamume aliyebadili jinsia yake na kuwa mwanamke kupitia msururu wa upasuaji mbalimbali alipeleka kwenye Instagram akilalamika kwa hedhi yake huwa na uchungu mno.
Akionekana kulalamikia maisha magumu na ya uchungu tele wanayopitia wanawake, Bobrisky alifichua kwamba wakati mwingine yeye hulia anapoona hedhi yake, akisema kuwa ni ya uchungu mkali.
“Kusema kweli sasa hivi najihisi kabisa kuwa mwanamke aliyekamilika. Wakati mwingine huwa navunjika kwa kilio wakati niko kwenye siku zangu za mwezi, kwa sababu ni uchungu sana,” Bobrisky aliandika.
Watumizi wa Instagram walifurika kwenye chapisho hilo wakimsuta vikali wengine wakihisi anawatania kuhusu siku za mwezi kwani yeye bado ni wa jinsia ya kiume hata kama anajitambua kama mwanamke kupitia upasuaji.
Haya hapa baadhi ya maoni;
Anthony Omoni alisema, "Wanaume walichukua mada ya mwaka "No gree for anybody. Mama wa Lagos ni mwanamume, mwanamke aliyevaa vizuri ni Mwanaume, binti wa kifalme wa Afrika ni mwanamume, Tinubu anafaa kumteua Mwanaume kama Waziri. wa Masuala ya Wanawake”.
Rietta aliuliza, "Hedhi ni kumwaga kitani cha tumbo kwa hivyo nimechanganyikiwa, je, wanaume pia wana tumbo?".
Muhammed Baaheer alibainisha, "Nasubiri kusikia ujauzito mwezi ujao kipindi hicho ambacho hutaona siku zako za mwezi".
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!