MALKIA wa muziki wa Reggae kutoka taifa la Jamaika,
Etana ameonyesha kutofuraiswa kwake baada ya shoo yake kugongana na shoo ya
Diamond Platnumz kupelekea kusitishwa.
Etana kupitia ukurasa wake wa X, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wenye nguvu ambao walihakikisha shoo yake haifanyiki licha ya kuanza kupigiwa debe miezi kadhaa iliyopita.
Mrembo huyo ambaye aliona shoo yake Jumamosi usiku ikipigwa breki, alisema kwamba kuna watu walihakikisha wanamkatisha tamaa kwa kuandaa shoo nyingine sambamba na yake.
Itakumbukwa shoo ya Etana ilijipata imeratibiwa wakati mmoja na shoo ya Furaha Fest ambayo mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alikuwa miongoni mwa wasanii wakuu kutumbuiza.
“Kuna mtu amelipa pesa nyingi kuhakikisha shoo yangu usiku wa leo inahujumiwa! Sifurahishwi na hujuma na niseme wazi sijitokezi kwenye show ya Diamond Platinumz!!!!! Yote ni poa,” Etana alisema kwa sehemu.
“Onyesho langu la Desemba. 7 lilikuwa likipigiwa debe muda mrefu kabla ya mtu kuibuka na onyesho la Diamond Platnum siku moja na katika eneo moja,” aliongeza.
Etana alisema kwamba alipokea kwa maskitiko makubwa kuwa shoo yake imetolewa kafara kwa ile nyingine kwani hakuna vile shoo zote mbili zingefanyika katika eneo vmoja.
“Kisha ghafla nasikia maonyesho mawili hayawezi kufanyika katika ENEO MOJA kutoka kwa mamlaka na show yangu usiku wa leo haiwezi kutokea.”
Mrembo huyo alihoji ni kwa nini yeyote anayejaribu kufanya hivyo anaogopa tu yeye mwanamke mmoja tu kwa kupanga ratiba ya wasanii wengine kutumbuiza.
“Siasa na maigizo haya yote kwa msichana mmoja. Nashangaa ni nani yuko nyuma ya yote. Kwa nini unaogopa show moja na mwanamke mmoja?” Alihoji.
Hata hivyo, baada ya shoo ya Etana kupigwa breki ghafla, taarifa zinadai kwamba Diamond pia hakuweza kutumbuizia mashabiki katika Furaa Fest na aliondoka jukwaani ghafla.
Msanii huyo anaarifiwa kuondoka Jukwaani baada ya kugongana na msanii wa humu nchini Willy Paul ambaye pia aliratibiwa kutumbuiza kabla yake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!