KIZAAZAA kilishuhudiwa katika ukumbi wa Polo jijini Nairobi ambapo shoo ya Furaha Fest ilikuwa imeandaliwa usiku wa Jumamosi ya Desemba 7.


Mashabiki wa Diamond Platnumz, mmoja kati ya wasanii wakubwa waliotarajiwa kupakua burudani walibaki na nyuso zilizosawijika baada yaq msanii huyo kukataa kutumbuiza.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Video ambayo ilionekana mahsusi na Radiojambo.co.ke ilionyesha jinsi zogo lilizuka baina ya Diamond na umati wa mashabiki pindi tu alipojitoma jukwaani.


Muda mfupi baada ya kuingia jukwaani, na hata kabla hajaanza kupakua burudani kwa mashabiki waliofurika, Diamond alipata mapokezi mchanganyiko, asilimia kubwa ya watu wakimfokea na kumnyoosea vidole.


Wengine walikuwa wanamfokea Diamond huku wakiimba jina la msanii wa humu nchini, Willy Paul kwa mbwembwe, jambo lililompa Diamond wakati mgumu kuendelea kutumbuiza.


Kwa ghadhabu, Simba – kama anavyojiita, aliondoka stejini akiwa amekatishwa tamaa na hivyo ndivyo hakuweza kutumbuiza licha ya mashabiki wengi kulipa gharama za juu kwa ajili ya kupata tumbuizo lake.


Inaarifiwa kwamba Diamond aliratibiwa kuwa wa mwisho kutumbuiza lakini upande wake ulisisitiza atumbuize kabla ya Willy Paul ambaye alikuwa atumbuize mwanzo.


Mfarakano huo ulisababisha ushindani wa kibabe baina ya masabiki wengi wa Willy Paul na wachache wa Diamond Platnumz, kumpelekea kuondoka ukumbini.


Hata hivyo, mpaka wakati wa kuchapishwa kwa ripoti huu, upande wa Diamond haukuwa umetoa tarifa yoyote kuzungumzia tukio hilo.


Kwa upande mwingine, Willy Paul – ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa sababu za Diamond kusitisha tumbuizo lake ametoa taarifa akisema kwamba alifanyiwa dhuluma katika hafla hiyo.


Pozee alihoji kwa nini Wakenya wanaruhusu kuonyeshwa madharau nyumbani huku wageni wakionyeshwa heshima.


“Ninadhulumiwa katika hafla hii, wanabadilisha ratiba dakika za mwisho, mbona Wakenya wanakubali ili kutokea? Wasanii wa Tanzania wanapewa kipaumbele katika hafla hii. Hii inasikitisha sana. Mbona Wakenya wanadharauliwa mbele ya Wabongo? Nitaendelea kupigania bendera hii, nitaifia bendera hii,” Pozee alisema huku akichapisha picha ya bendera ya Kenya.


Inasubiriwa kuonekana jinsi waandalizi wa Furaha Fest watashughulikia malalamishiv haya, haswa kutoka kwa mashabiki ambao baadhi wanahisi hawakupokea burudani jinsi walivyoptarajia baada ya Diamond kufeli kutumbuiza.