MWANZILISI wa kampuni ya usafiri wa watalii, Sarah Mtalii – awali akiitwa Sarah Kabu – ameomba msamaha kwa ushauri wake tata kwa wanawake kutoiasi ndoa licha ya manyanyaso.


Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati alikuwa akizungumzia kubadili jina lake kutoka Sarah Kabu kwenda kwa Sarah Mtalii, alisema kwamba baada ya kukaa chini ya kuitathmini hali, anaona kabisa ushauri huo haukufaa.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Sarah alisema kwamba kwa kuangalia hali ambayo anaipitia kwa sasa, anahisi kabisa kwamba ushauri wake ulikuwa mbaya kuwataka wanawake kukwama kwenye ndoa licha ya manyanyaso.


“Ninataka kuomba msamaha pia, kwa kuwaambia wanawake kukwama kwenye ndoa ambako kuna usaliti. Kina mama, tafadali naomba mnisamehe. Kama mambo hayaendi vizuri, tafadhali fungasha na uondoke ungali bado hai,’ Sarah alisema.


“Hivyo mimi ninaomba msamaha kwa kina mama, kwa kuwaambia make katika ndoa ambazo usaliti umekithiri. Kuanzia leo kwendelea mbele, kama hifanyi kazi, haifanyi kazi, wewe ondoka tu, ahsanbteni,” Sara aliongeza.


Kauli zake zinajiri wakati ambapo kuna sekeseke mitandaoni kuhusu kukosekana kwa maelewano baina yake na mume wake Simon Kabu ambaye sasa anasema hawako pamoja.


Wawili hao wamekuwa wakirushiana vijembe mitandaoni, Sarah kwa wakati mmoja akiitaka idara ya DCI kufanya uchunguzi kuhusu kile alichodai ni kufanyiwa dhuluma katika ndoa yake.


Simon kwa upande wake alifanya video ya kusimulia jinsi mfarakano wao ulianza, akisema kwamba alilazimika kufanya video hiyo kusikika upande wake kwani wakati mwingine kunyamaza kunatafsiriwa kama kukubali lawama.


Msahama wake umetokea wiki chache tu baada ya kuzua mgawanyiko mitandaoni kwa kusema kwamba ku’cheat hakufai kuwa sababu pekee ya mke kuivunja ndoa yake.


“Ningependa tu kuwadokezea wanawake kwamba haya mambo hutokea. Kila wakati ninapata content yenye naweza chanua wanawake, huwa muda wote naipakuwa kwao.”

“Siku hizi mimi huwaambia wanawake, kwa kweli kuchepuka hakufai kuwa moja ya sababu yetu kuwaacha wanaume au kuanza kuwa na wasiwasi kuhusu wanaume wetu. Hebu acha tuwe na mashaka kuhusu vitu vingine vikubwa kuliko kuwa na mashaka iwapo anachepuka au la,” Sarah Kabu alisema.