Mwanahabari wa muda
mrefu katika tansia ya Habari za ufichuzi, John Allan Namu ametupwa kwenye
dimbwi la majonzi na maombolezo kufuatia kifo cha mamake.
Namu alitaarifu umma Habari hizo za kuvunja moyo kupitia ukurasa wake wa X ambapo alichapisha picha ya mamake na kuifuatisha kwa maneno ‘kwaheri mama yangu mpendwa’ kwa lugha ya Kikuyu.
“Koma wega mami wakwa ?” Namu aliandika.
Watu mbalimbali wamemfariji mwandishi huyo wa Habari za ufichuzi ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa African Uncensored.
Hizi hapa ni baadhi ya jumbe za kumfariji kutoka kwa watumizi wa mtandao wa X;
‘Pole sana John. Upate amani na ufahamu katika nyakati hizi za majaribu.’ Ayiela Lucia alimwambia.
‘Pole sana kwa hasara yako. Mungu aipe familia yako pumziko katika kipindi hiki kigumu’ Shawrie for Rx aliandika.
‘Rambirambi zangu kwenu na familia zenu. Pole kwa hasara. Mungu akupe nguvu na uwezo wa kubeba hasara.’ Wajulia alisema.
Hata hivyo, Namu hakuweza kufichua Chanzo cha kifo cha mama yake.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!