MSANII nambari moja wa injili ya kizazi kipya nchini Kenya, Guardian Angel amefichua kwamba hakuaqnza muziki tu na kupata umaarufu kwa wakati mmoja.


Akizungumza na mtengeneza maudhui, Dem wa Facebook alipomtembelea nyumbani kwake Karen, Guardian Angel alisema kwamba watu wengi wanafikiria wanaweza anza kufanya kitu leo na kuwa maarufu katika muda huo.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Japo alikiri kwamba hiyo ipo, lakini alisema ni kwa watu wachache, akijitolea mfano kwamba yeye ni miongoni mwa wale waliotembea safari ndefu ya muziki kabla ya kuja kupata mafanikio kutoka kwa muziki wenyewe.



“Unajua watu wanadhania hivi vitu kwenye maisha ni kuamka leo na unawahi. Halafu kitu kingine watu husahau ni ku’appreciate. Mtu anadhani tu ni bed of roses kuamka na kufanya rocket science na kuwa supastaa, kesho kutwa uko na pesa…hawajui hii ni kitu mtu unajenga hatua kwa hatua,” Guardian Angel alisema.


Angel alifichua kwamba yeye alianza kufanya muziki 2009 na 2011 ndio mwaka aliachia iwmbo wake wa kwanza rasmi lakini matunda matamu ya muziki alianza kuyachuma mwaka 2018.


“Unajua mimi nime’hit 2018 na wakati huo nilikuwa nimeanza muziki 2009. 2011 ndio nimetoa wimbo wangu wa kwanza lakini ngoma zingine nilikuwa nimesharekodi. Nikakuja nikatoa wimbo wa kwanza rasmi 2011 lakini nilikaa miaka 7 bila kupata hit. 2018 ndio wimbo wangu wa kwanza ‘Nadeka’ ulikuwa maarufu.”



“Sasa kutoka hapo ndio nyimbo zingine zikatokea, unaona. Ni ukuaji wa kujikokota na si kitu unaamka leo kesho umekuwa staa,” Guardian Angel alisema.


Akijibu kuhusu ni kwa nini yeye amekwama kwa injili kwa muda mrefu, tofauti na wasanii wengine ambao huanza na injili na baadae kuhamia sekta ya miziki ya kidunia, Angel alisema kwamba yeye alianza uimbnaji kama tayari anamjua Mungu.


“Mimi nikianza usanii, tayari nilikuwa nimeokoka. Nilikuwa nampenda Mungu kwanza, nikawa na uhusiano mzuri na Mungu ndio nikaanza kuimba. Mimi ndio maana unaona siwezi imba sekuloa juu sijui kuelezea mapenzi, wasichana jinsi walivyo. Hiyo itanishinda. Unajua hizo nyimbo zinataka ujue kusema hivyo vitu,” Angel alisema.