MKUSANYIKO wa mashabiki wa Arsenal kusherehekea ushindi wa timu yao dhidi ya wapinzani wa jadi, Manchester United nchini Uganda uligeuka na kuwa vilio baada ya risasi kufyatuliwa kuwatawanya.


Tukio hilo lililoripotiwa na Nile Post lilitokea usiku wa Jumatano katika wilaya ya Kalungu mji wa Lukaya ambapo mamia ya mashabiki wa Arsenal walikuwa wanamenyana kwa maneno na wenzao wa Man Utd.


Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Hapo ndipo mlinzi wa kibinafsi alifyatua risasi kutawanya makabiliano hayo ambayo yalikuwa yanaelekea kuhamia kwenye vita kutoka kwa maneno.


Mlinzi wa Kampuni ya Gardaworld Security anadaiwa kufyatua risasi huku hali ya wasiwasi ikiongezeka wakati wa sherehe za mashabiki wa Arsenal.


Tukio hili ni mwaka wa pili mfululizo ambapo mechi kati ya wababe hawa wawili wa soka imezua hisia kali mjini Kampala.


Mwaka jana, ushindi wa Arsenal uliripotiwa kusababisha kujitoa uhai, kudungwa kisu na kukamatwa kwa mashabiki saba waliokuwa na furaha katika Jiji la Jinja kwa kufanya gwaride la dhihaka la kombe.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, meneja wa jengo hilo aliyetambulika kwa jina moja la Banda, alijibizana na mashabiki hao wakiimba na kushangilia na kumuagiza mlinzi huyo kuingilia kati.


Licha ya onyo nyingi, mashabiki waliendelea na sherehe zao. Katika jaribio la kurejesha udhibiti, wamiliki wa jengo hilo walizima umeme, ambayo ilizidisha hali tayari tete.


Katikati ya machafuko hayo, mlinzi huyo anadaiwa kuachia bunduki yake na kumjeruhi vibaya John Ssenyonga mwenye umri wa miaka 30 na kumjeruhi shabiki mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Lawrence, Nile Post walibaini.


Ssenyonga alifariki dunia kwa majonzi katika eneo la tukio. Msemaji wa Polisi Masaka, Twaha Kasirye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa upelelezi unaendelea na kesi imefunguliwa dhidi ya mlinzi huyo ambaye kwa sasa anatafutwa na mamlaka.


Kasirye aliwataka mashabiki wa soka kujizuia wakati wa sherehe, akisisitiza kuwa vurugu kwa jina la soka hazikubaliki.


Tukio hili limezua taharuki kwa Lukaya, huku wakazi wakidai uwajibikaji na kutilia shaka vitendo vya wanausalama binafsi.


Wasiwasi umekuzwa kuhusu matumizi ya nguvu hatari katika mazingira ya kiraia, haswa wakati wa sherehe isiyo ya vitisho.


 Janga hilo limezidisha wito wa udhibiti mkali na uangalizi wa kampuni za usalama za kibinafsi.