Kasisi mmoja wa kanisa Katoliki amezua mjadala mkali
mitandaoni kuhusu idadi kubwa ya matangazo ya injili kwenye mabango ya biashara
barabarani kuliko idadi ya mabango ya
viwanda.
Kasisi huyo kwa jina Fada Angelo Chidi Unegbu, alisema kwamba nchi yenye idadi kubwa ya mabango yanayotangaza injili na wokovu kuliko ajira ni nchi inayotumbukia kwa umaskini.
Alisema kwamba nchi yenye injili kupita kiasi bila viwanda vya kutoa ajira ni nchi ambayo itakosa usalama na kutomucha Mungu.
Alitumia ukurasa wake wa Facebook kutoa madai hayo yenye utata.
Kulingana na kasisi huyo, ikiwa nchi ina mabango mengi ya kutangaza dini, badala ya biashara, nchi kama hiyo itakuwa imeshinda tu katika bidhaa za kidini.
Maneno yake…
“Nchi ambayo ina mabango mengi ya kidini kuliko mabango ya viwanda au matangazo haiwezi kusemwa kuwa ya kidini. Badala yake ni nchi ambayo imebobea katika biashara za kidini. Nchi kama hiyo itasalia kuwa maskini, isiyo salama na isiyomcha Mungu.”
Kauli yake inajiri wakati ambapo mataifa mengi ya Kiafrika yamejikuta katika hali ambapo wachungaji wengi wamefurika kila kona mijini na vijijini katika kile wanasema ni ‘kueneza injili ya wkovu.’
Katika chapisho hilo, watu walitoa maonim, wengi wakionekana kukubakiana na kasisi huyo kwamba nchi zilizoendelea zina idadi ndogo ya matangazo na maeneo ya kuabudu.
“Ninalaani udini uliokithiri, lakini baadhi ya nchi za Ulaya zimetoa wachungaji na WAINJILI wengi kuliko Afrika nzima,” Evangelist Drlingtone Igboke alisema.
“Mambo mengi sana yataharibika kama jambo sahihi halijafanyika...ikiwa serikali itatengeneza ajira leo d shughuli za bidhaa hizi zote za kidini zitapungua sana. Ukosefu wa kazi umewalazimu watu wengi kujiita manabii na manabii,” Rita Chinaza alisema.
“Hadi watu wakubali ukweli huu mchungu, kizazi kijacho kitaendelea kutumainia tahadhari ya miujiza na pesa kwa kuinua simu zao katika zile zinazoitwa vituo vya uuzaji viitwavyo miujiza centers.” Albanaheart tv aliongeza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!