BOSI wa lebo ya WCB
Wasafi, Diamond Platnumz amerejea kwa Mungu na kilio cha pekee akiomba ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa
Instagram, msanii huyo aliandika ujumbe wa kumlilia Mungu akimuomba kumbariki
na ndoa katika kile alisema kuwa amechoka kuishi maisha ya ukapera.
Akionyesha mafadhaiko
yake, Platnumz alisema kwamba japo hajui mipango ya Mungu katika maisha yake,
lakini pia angependa Mungu kumujumuisha katika orodha ya wale atakaowabariki na
ndoa ya kudumu.
“Ewe Mungu, sijui mipango yako kuhusu maisha yangu ni ipi lakini kusema ukweli nimechoka kuishi maisha bila mke. Tafadhali nibariki na ndoa,” Platnumz alimuomba Mungu.
Ombi lake linakuja siku chache tu baada ya Zuchu – anayetajwa kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz kutangaza kwa mara nyingine tena kwamba uhusiano wao umefariki dunia.
Zuchu katika chapisho lake, alisema kwamba amechoka na mapenzi ya Diamond na kumtakia kila la heri katika maisha yake bila yeye.
“Baada ya miaka 3 ya kuchumbiana, Diamond na mimi tumeamua kutia nanga katika penzi letu. Huu ni uamuzi wa pamoja na tunasalia kuwa marafiki wa karibu,” Zuchu alisema.
Hata hivyo, baadhi walihisi hii ilikuwa njia moja ya Zuchu kutafuta kiki, jambo ambalo alilikanusha vikali.
“I know mimi ni maarufu na kuongelewa ni kawaida. But kindly msipitilze kunipa sifa za uongo mradi kumpamba boss haswa kwa media ya nyumbani ambayo mnaweza pia kupata ukweli wa mambo mkasawazisha stori zenu,” Zuchu alilalamika kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Aliendelea, “Hii ndio sababu hasa kwa nini niliondoka, unachoka kuwa na mwanaume anayekusukuma kwa watu utukanwe na yeye ndo anayetumika kwenye kudhalilika kwako. Mwanamke wake ndo kanyagio la kila aliyemzunguka , akiamua tu basi yeye huungana nao na kuwapa vichwa vya kunivunjishia heshima ilhali umekaa kimya na unachofanya tu ni kukaa na kumeza. Ninajaribu kuwa mtu mzuri na kiungo dhaifu katika maisha yangu ni yeye."
Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kutangaza kuachana na kufanya vimbwanga mitandaoni na baadae kuonekana pamoja.
Kuachana kwao kunajiri siku kadhaa baada ya Zuchu kutumia fursa za kutumbuiza pamoja na Diamond jukwaani kumuuliza ni lini atamuoa rasmi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!