Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeipiku Kenya kwenye msimamo wa jedwali la soka
duniani, FIFA.
Tanzania ilijiimarisha kwenye jedwali hilo baada ya kupanda juu nafasi 6 zaidi huku
Kenya ikiporomoka kwa nafasi 2 chini zaidi.
Kenya ambayo awali ilikuwa katika nafasi ya 106
duniani iliporomoka hadi nafasi ya 108 huku Tanzania ikipanda kutoka nafasi ya
12 duniani hadi nafasi ya 106.
Haya yanajiri baada ya Harambee Stars kukosa kushinda
mechi zao mbili zilizopita dhidi ya Zimbabwe na Namibia mtawalia.

Pia walishindwa kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco, huku Tanzania ikiifunga Guinea 1-0 na kufuzu
kwa michuano hiyo ya bara Afrika.
Mnamo mwezi wa Novemba, Kenya ilisajili sare tatu -
sare ya 1-1 na Namibia na Sudan Kusini (Kufuzu kwa CHAN) na sare tasa dhidi ya
Zimbabwe ambayo iligonga hatma ya Kenya ya kutofunga safari yao ya AFCON kwenda
Morocco mwaka ujao.
Kenya imekuwa ikifanya vibaya zaidi katika mashindano
mbalimbali mwaka huu, hali ambayo imehusishwa na timu ya taifa kuchezea
michuano yake mingi nje ya nchi.
FIFA na CAF walikataa kuidhijmisha viwanja vyote vya
Kenya kutumika katika michuano ya kufuzu kombe la dunia na AFCON katika kile
walisema kwamba viwango vya viwanja vyote vikuu vya Kenya ni duni.
Kenya ilichezea mechi zao za nyumbani kufuzu kombe la
dunia nchini Malawi mapema mwaka huu huku pia wakitumia viwanja vya Uganda na
Afrika Kusini kushiriki mechi za kufuzu AFCON 2025 ambayo walifeli.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda bado ndiyo
timu iliyoorodheshwa bora kwenye nafasi ya 88 ikifuatiwa na Tanzania iliyo na
106 na Kenya 108.
Uganda na Tanzania zimefuzu kwa AFCON 2025
itakayofanyika Morocco kuanzia Jumapili, 21 Desemba 2025 hadi Jumapili, 18
Januari 2026.
Timu 5 bora duniani kwa wakati huo hazijabadilika,
huku Argentina bado ikiorodheshwa kuwa timu bora zaidi Duniani. Ufaransa,
Uhispania, Uingereza na Brazil wanakamata nafasi nyingine tano za juu mtawalia.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!