AFISA mkuu mtwendaji wa halimashauri ya hatimiliki za
kazi za Sanaa humu nchini MCSK, Ezekiel Mutua ametupwa katika kipindi cha
maomboleza baada ya kufiwa na baba.
Mutua alitoa taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa
Facebook ambapo alichapisha picha ya pamoja na mkongwe huyo ikionekana ni
majira ya jioni.
Akimuomboleza, alisema kwamba atakachokikosa zaidi ni
nyakati hizo za jioni ambapo mara kwa mara wangejumuika kwa soga humu wakiaga
kutwa.
“Jioni
kama hizo hazitakuwa tena, lakini katika kila kitu tunashukuru na kuthamini
kumbukumbu nzuri. Nimepoteza rafiki mkubwa. Nenda salama baba. .
.” Ezekiel Mutua aliandika.
Kifo cha baba kimetokea takribani miaka 2 tu baada ya
mamake kufa.
Akiarifu kuhusu kifo cha rafiki yake wa karibu –
mama, Mnamo Februari mwaka jana, Mutua alisema kwamba alimpoteza mmoja wa
mihimili mikuu katika maisha yake.
Baade alionekana kufululiza machapisho ya jinsi
amekuwa akikaa karibu na mzee babake ili kumfariji, akisema kwamba ni Dhahiri kifo
cha mamake kilimuathiri sana babake.
Katika sasisho jingine, Mutua japo kwa kumuombileza,
alimsherehekea babake na kumshukuru Mungu kwa kuipa familia fursa ya kuishi
naye hadi umri wa miaka 100.
Alifichua kwamba babake ni mmoja kati ya watu
wachache walio hai hadi leo hii na ambao walishuhudia kutokea kwa vita vya
kwanza na pili vya dunia.
“Sio
wengi wanaopata fursa ya kufikisha miaka 100 na kuondoka duniani wakiwa
wamezungukwa na wajukuu wao wakuu. Baba aliona Vita vya Kwanza na vya Pili vya
Dunia na ameshuhudia takriban njaa na magonjwa ya mlipuko katika historia
iliyorekodiwa.”
“Kuondoka
kwa baba ni chungu lakini ameacha urithi wa hali ya juu,”
Mutua aliongeza huku akinukuu kifungu cha Biblia kitabu cha Ayubu.
Kifo cha babake kinatokea wakati ambapo Mutua
anapitia wakati mgumu katika ofisini yake baada ya baadhi ya watu waliodaiwa
kuwa wanachama wa MCSK kutoa taarifa kwamba amesimamishwa kazi kama bosi wa
halimashauri hiyo.
Hata hivyo, ni barua ambayo Mutua aliipuzilia mbali siku moja baadae, aliitaja kama propaganda mbaya ambayo inaendeshwa na watu aliowazuia kuingia katika afisi za MCSK bila itifaki inayofaa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!