Joe Waithira



Murang'a Seal iliilaza Sofapaka 1-0 na kukwea hadi nafasi ya nane kwenye orodha ya Ligi Kuu ya Kenya baada ya kukaa muda mwingi wa msimu kwenye eneo la hatari.

Joseph Waithira alipachika wavu bao la pekee katika mechi hiyo ya kusisimua ugani Dandora siku ya Alhamisi.

Hili lilijiri baada ya kipa wa Sofapaka Brandon Obiero kumpiga kiwiko John Mwita ndani ya kisanduku, na kumfanya mwamuzi wa kati kuelekeza penalti.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

 Kulikuwa na sherehe zisizo na sauti kufuatia bao hilo, Waithira aliponyanyua shati iliyoandikwa ‘Ma Chloe 01’.

Ishara yake iliashiria heshima kwa kipa wa Murang’a Seal Wilson Ngamau aliyefiwa na mkewe wiki jana.

 Ushindi wa vijana hao wa Juma Abdallah ulikuwa wa maana sana, kwani ulikipandisha kikosi chake kutoka nafasi za kushuka daraja hadi nafasi ya nane.