
Wanasheria kote nchini Kenya na nje ya nchi wanaendelea kuomboleza kifo cha wakili Dkt. Wilfred Mutubwa aliyefariki ghafla baada ya kuzirai akiwa afisini mwake mjini Nairobi siku ya Jumanne.
Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya Faith Odhiambo ametuma risala za rambirambi kwa familia na marafiki wa Wakili Mutubwa. Odhiambo alielezea kifo cha Mutubwa kama "hasara kubwa" kwa taaluma ya uanasheria na kusherehekea mchango wake kukuza taaluma hiyo”.
Rais wa LSK alisema ushawishi wa Mutubwa kwa taaluma ya sheria, wasomi, na jamii pana utaendelea kuguswa katika maisha ya wale wote aliowashauri, kufanya kazi nao na kuwatia moyo.
Kulingana na ripoti za polisi Dkt. Mutubwa alikuwa afisini mwake akihudhuria kikao cha mahakama alipoanguka walipokuwa wakienda kwa mapumziko mafupi katika ofisi iliyo karibu na Hospitali ya Nairobi.
Kufikia kifo chake Dkt Mutubwa alikuwa Mkuu wa idara ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Mount Kenya. Pia alikuwa gwiji aliyetambulika kote duniani kwa Usuluhishi Mbadala wa Mizozo baada ya kuhudumu kama Mwenyekiti wa Taasisi ya Waamuzi wa Chartered - Kenya. Pia alikuwa akihusika katika utatuzi wa mzozo katika Hospitali ya Nairobi na alikuwa akifanya juhudi kusuluhisha mvutano huo.
Marafiki na wenzake waliosoma naye katika shule ya upili ya Musingu akiwemo Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna walimbikizia sifa wakili Mutubwa kama mtu mwenye busara na ambaye alithamini urafiki.
Meza ya habari ya Radio inaitakia risala za rambi rambi familia ya Dkt. Wilfred Mutubwa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!