MWIMBAJI maarufu wa Afrobeats kutoka Nigeria, Patoranking hatimaye amezungumza baada ya kifo cha dada yake, Chioma na mumewe.

Patoranking alivunja kimya chake kupitia ukurasa wake wa Instagram, siku chache baada ya kuwazika wawili hao ambao waliripotiwa kufariki katika mkasa wa mlipuko wa moto nyumbani kwao

Vyabzo vya habari za burudani kutoka taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika viliripoti kuwa tukio hilo lilitokea siku moja baada ya sherehe yao ya kuwapa nyumba.

Wenzi hao walizikwa Jumamosi, Novemba 23 2024, katika jimbo la Ebonyi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Walakini, akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya tukio hilo, Patoranking katika chapisho kwenye hadithi yake ya Instagram mnamo Jumatatu, Novemba 25, aliandika, "mbingu pekee ndiyo inajua."

Taarifa za Patoranking kufiwa na dadake na shemeji yake kwa wakati mmoja zilizagaa mitandaoni miezi mitatu iliyopita ambapo shughuli za mazishi zimejikokota kwa zaidi ya siku 90.

Jirani alisimulia mlipuko huo, akisema, "Ilitokea mtaani kwangu. Tulisikia tu mlipuko huo alasiri. Tulipokimbilia eneo la tukio, moshi ulikuwa ukifuka kutoka kwenye jengo jipya. Vifaa vyote vya kielektroniki viliharibiwa, na dari, milango, madirisha, na vioo viliharibiwa vibaya sana.”

Chioma Onuabuchi, dadake Patoranking aliaga dunia kwa kutokana na majeraha yake mnamo tarehe 31 Agosti, huku mumewe George Onuabuchi akifuata kwa huzuni Septemba 11.

Wanandoa hao waliacha nyuma mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye kwa bahati nzuri alikuwa na bibi yake wakati wa tukio hilo.

Mazishi ya Chioma na George yalifanyika Jumapili, Novemba 24, 2024.

Ilikuwa tukio chungu kwa mwimbaji na familia yake. Kumbuka kwamba Patoranking alisherehekea dada yake na mumewe siku ya harusi yao mnamo 2021 na zawadi mpya ya gari.

Msanii huyo wa kibao cha Abule aliandika chapisho lake la mwisho kwenye Instagram mnamo Agosti 20, 2024, na mashabiki walichukua muda kwenye mitandao ya kijamii kumuhurumia yeye na familia yake.