
MSANII mmiliki wa lebo ya Bad Nation, Marioo
amefunguka sabbau ya yeye na mwenazake wa Konde Gang, Harmonize wanapenda
kuimba nyimbo za mapenzi na kuumizwa kimapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kudokeza
ujio wa ngoma nyingi za kolabo na Harmonize, Marioo alisema kwamba wote wawili
huwa wanaendana sana katika mtiririko pindi wanapoingia kwenye studio kurekodi.
Alikiri kwamba yeye na Harmonize ni wasanii wakali
ambao siku zote wakikutanisha ukali wao wa cheche, moto unakuwa wa kipekee.
“Mimi
na Harmonzie, kwanza sisi wote wakali, kwa hiyo cheche zikikutana lazima
zitengeneze moto mkubwa. Na ndio maana mipango yote tunapanga wakati wa kazi
inafanikiwa. Huwa tunakaa, tunapanga tunatoa wimbo na pia tunasaidiana
kuisukuma.”
Marioo alimsifia Harmonize kuwa ni msanii wa kipekee
katika uandishi wa mashairi ya Kiswahili na haswa katika midundo ya Bongo
Fleva.
“Sisi
tunapenda kuimba hizo nyimbo. Tunapenda Bongo Fleva, tunapenda kuimba nyimbo za
mapenzi na kuumizwa kwa sababu tunaziweza sana. Lakini kinachosababisha hivi
vyote nafikiri ni chemistry tu. Unaeza kuta wasanii wengi ni wakali lakini kama
hawana chemistry ya aina Fulani vile,” alisema.
Marioo alisisitiza kwamba heshima yake kwa Harmonize
haiwezi kupimika kwa mizani ya dunia hii, akimiminia sifa kwa kufanikisha
kolabo yao ya kwanza ‘Naogopa’ kuwa sauti kubwa ambayo mkapa sasa inasimika
jina la wawili hao kwenye rubaa za kolabo bora za muongo katika Bongo Fleva.
Marioo alitumia mahojiano hayo kunyoosha maelezo
kuhusu uvumi wa kuwepo kwa bifu kati yake na aliyekuwa mcheza densi wake, Chino
Kidd.
Marioo alisema kwamba kinyume na dhana pana kuwa hawapatani,
yeye na Chino na marafiki wa karibu ambao Amani imetawala kati yao.
Msanii huyo alipoulizwa kama anahisi amechangia
katika maisha ya mafanikio ya Chino Kidd, alisema kwamba yeye anahisi kabisa
kwamba anachomiliki ni chake kwa sababu pia anafanya kazi kwa bidii kama msanii
wa Amapiano ya Kiswahili.
Chino na Marioo walipapurana kwenye mitandao ya kijamii wiki kadhaa zilizopita, Marioo akimtuhumu Chino kwa kujaribu kumtilia sumu ili kumuua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!