November 26, 2024
2 min read

Siku
ya Jumatatu, kijana aliyepinga kwa sauti kubwa kuuzwa kwa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) wakati wa maandamano ya kitaifa katikati mwa
mwaka, Henry Omondi, alitua jijini Nairobi kutoka Kaunti ya Siaya ambako
amekuwa akiendelea na masomo ya kiufundi.
Kijana
huyo alipata fursa ya maisha yake kwani alitua mjini kwa njia ya anga. Ilikuwa
ni mara yake ya kwanza kabisa kupanda ndege na kutua katika JKIA.
Mchekeshaji
Eric Omondi aliandamana naye kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu hadi
JKIA, kabla ya kuendelea na mambo mengine jijini.
“Ndugu
yetu leo Amepanda ndege na kutua JKIA kwa mara ya kwanza kabisa.
Tunasherehekea na kumthamini,” Eric alisema.
Walipofika
Nairobi, Henry alipelekwa kukutana na Mbunge wa Githunguri Gathoni wa Muchomba
ambaye alimuuliza kuhusu safari yake ya ndege.
Enjoying this article?
Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans
“Ndege
ilikuwa poa. Tumefika poa kwa neema ya Mungu,” Henry alisema.
Mwanasiasa
huyo alimshukuru Eric Omondi kwa kumsaidia kijana huyo kutoka mtaani na
kumsajili katika chuo cha Ndere Polytechnic kwa kozi ya umekanika.
Gathoni
pia aliahidi kumpeleka kwa ununuzi na kumnunulia vitu anavyohitaji ikiwa ni
pamoja na nguo na vitu vya sikukuu ya Krismasi.
“Nataka
kutengeneza maneno ya sikukuu. Si unaona ata viatu hatuna. Hatuna kiatu ya
kukaa huku Nairobi sababu tuko na moja tu ya shule, na imebaki shule. Haiko
sura nzuri vile. Pia huyu kijana anahitaji kununuliwa nguo,” Gathoni Wa
Muchomba alisema.
Aidha,
Gathoni pia aliahidi kutengeneza meno ya Henry, miongoni mwa mambo mengine
ambayo hayajafichuliwa iwapo atapata kibali chake.
“Huyu
kijana nataka tutengeneze (meno) akinipatia ruhusa. (Akimuangalia Henry) Si
tumesema tutatengeneza meno, unataka tutengeneze?.. Tumekubaliana tutatengeneza
meno tuwe wanaume poapoa. Si mnaelewa. Alafu maneno mengine yetu ambayo
yanatangaza hapa, Maneno ya mama na kijana tutatengeneza,” alisema.
Mbunge
huyo pia aliahidi kumsaidia Henry katika masomo yake na kumshauri anapokua.
"Ninajitolea
kusaidia (elimu ya Henry) hadi kukamilika. Kwa hivyo sasa tufanyie kazi urembo
wake wa kibinafsi na kumpa uwekezaji wa baadaye tunapomshauri kuwa mwanamume
halisi. Wacha kazi ianze tukimmaliza,” alisema.
Pia
aliwaomba watu wenye mapenzi mema ambao wangetaka kumsaidia Henry kuwasiliana
naye au mchekeshaji Eric Omondi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!