
MWANASOSHOLAITI na mfanyibiashara wa bidhaa za urembo
Huddah Monroe kwa mara nyingine tena amejibu kuhusu uvumi wa kuwa mwanachama wa
iluminati.
Akizungumza na mashabiki wake kupitia kipindi cha
maswali na majibu kwenye Instagram, Monroe aliulizwa na shabiki mmoja kutangaza
msimamo wake ikiwa ni mwanachama wa iluminati au la.
Monroe alijibu waziwazi kwamba angekuwa kwenye
jumuiya hiyo asingekuwa anahangaika kuzumbua riziki usiku na mchaka siku 7 za
wiki.
Kauli yake ilitengua dhana kwamba wanaokuwa wanachama
wa iluminati huwa na ukwasi wa ghafla ambao hawakuufanyia kazi.
“Wewe
ni mwanachama wa iluminati?” shabiki alimuuliza.
“Natamani
ningekuwa, kwa sababu nisingekuwa nafanya kazi kwa bidii hivi,”
Monroe alijibu.
Hii si mara ya kwanza kwa suala la kuwa kwenye
iluminati linaibuliwa dhidi ya mfanyibiashara huyo.
Miezi kadhaa iliyopita alipobadilisha picha ya
utambulisho kwenye ukurasa wake wa Instagram, Huddah alilazimika kuwafafanulia
mashabiki wake maana ya picha hiyo ambayo wengi waliihusisha na nembo ya
jumuiya ya iluminati.
Monroe alisema kuwa picha hiyo yenye jicho ni jicho
lenye nguvu kuu linalomuangalia muda wote kutoka juu.
Pia mwezi Julai mwaka huu, Monroe aliwashangaza wengi
alipokiri kwamba akatakiwa kuchagua kati ya Ukristo na iluminati, angechagua
iluminati akiwatuhumu Wakristo kwa kuwa vigeugeu na waongo.
Kupitia mfululizo wa hadithi za Instagram, Huddah
Monroe, ambaye wakati huo alikuwa amefichua kuwa ana mipango ya kufungua
kanisa, aliwashutumu waumini wa kanisa kuwa waongo.
"Kwa wakati huu, ningechagua Illuminati kuliko
Mkristo. Waumini wote hawa ni waongo,” alisema.
"Wote huenda kanisani na pesa zetu hupotea."
Awali, mwanasosholaiti huyo ambaye mara nyingi
huonekana jijini Dubai alifichua kwamba ana mpango wa kurejea nchini Kenya
mwaka 2026 na kuanza mchakato wa kueneza injili.
"Kwa
wale wanaoshangaa, ninarudi 2026 kufungua kanisa. Roho mtakatifu ndiye
aliyeniita,” akaeleza.
“Kama
wewe ni mchungaji chipukizi au nabii, nitakuajiri shikilia Biblia yako na
uisome. Waislamu pia wanakaribishwa kwenye ‘Huddah Prosperity Church’. Mahali
panapokupa utulivu wa akili na kubadilisha maisha yako kutoka 0-100,”
Monroe alitangaza.
Huddah Monroe alishiriki misheni na kauli mbiu ya
kanisa na kusema kanisa lake litaleta mabadiliko chanya na ushirikiano wa
vijana.
“Kauli
mbiu ya Kanisa la Huddah Prosperity ‘Kubadilisha Maisha’ au inaweza kuwarudisha
vijana kwa Mungu na mafundisho yake. Tutajadiliana,”
Monroe aliongeza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!