MOHAMED SALAH ameweka shinikizo kwa Liverpool kumpa mkataba mpya, akisema "kwa sasa anahisi yuko zaidi katika kuondoka kuliko kusalia".

Salah, 32, alifichua kuwa bado hajapewa kandarasi mpya, huku mkataba wake wa sasa ukikamilika msimu wa joto.

Salah alifunga mabao mawili dhidi ya Southampton Jumapili na kuifanya Liverpool kuwa mbele kwa pointi nane kileleni mwa jedwali kabla ya kufichua masikitiko yake ya kutopewa ofa.

Alisema: "Sawa, tunakaribia mwezi wa Desemba na sijapokea ofa yoyote ya kusalia kwenye klabu. Pengine niko nje zaidi kuliko ndani.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Sitastaafu hivi karibuni kwa hivyo ninacheza tu, nikizingatia msimu na ninajaribu kushinda Ligi Kuu na ninatumai Ligi ya Mabingwa pia.”

"Nimekata tamaa lakini tutaona."

Salah aliongeza: "Nawapenda mashabiki, mashabiki wananipenda, mwisho haiko mikononi mwangu au mikononi mwa mashabiki, tusubiri tuone.

"Unajua nimekuwa katika klabu kwa miaka mingi, hakuna klabu kama hii. Lakini mwishowe, hatima haiko mikononi mwangu. Ni Desemba na sijapokea chochote kuhusu mustakabali wangu."

Kuna hamu kubwa ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri kutoka Saudi Pro League, huku Liverpool wakiwa wamekataa ofa za hadi pauni milioni 150 hapo awali.

Alipoulizwa kuhusu matarajio ya kuhamia Mashariki ya Kati, alisema: "Sitaki kuzungumza juu ya hilo.

"Ninalenga na timu sasa. Mimi ni mtaalamu sana. Kila mtu anaweza kuona maadili yangu ya kazi. Najaribu tu kufurahia soka langu na nitacheza katika kiwango cha juu kwa muda mrefu iwezekanavyo.”

"Ninafanya kila niwezalo kwa sababu hivi ndivyo nilivyo na ninajaribu kutoa yote kwa ajili yangu na kwa ajili ya klabu. Tutaona kitakachofuata."

Salah ni mmoja wa wachezaji watatu muhimu ambao kandarasi yao itamalizika Anfield msimu wa joto, pamoja na Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold.

Van Dijk alifichua hivi majuzi kwamba mazungumzo yameanza kuhusu kandarasi mpya, wakati Alexander-Arnold amenyamaza kabla ya Real Madrid - ambao watatembelea Merseyside katika Ligi ya Mabingwa wiki hii.

Salah ana mabao 223 na asisti 99 katika mechi 367 alizoichezea Liverpool.