
Mkufunzi mkuu wa klabu ya KCB, Patrick Odhiambo, amesema vijana wake wamejiandaa vilivyo kwa mechi yao ya Ligi Kuu ya Kenya dhidi ya Talanta.
Timu hizo zitachuana katika uwanja wa Dandora jijini Nairobi siku ya Ijumaa. Wanabenki hao wananuia kuimarisha uongozi wao kileleni mwa jedwali.
Kufikia sasa KCB imezoa alama 17 baada ya kushinda mechi tano, kucheza sare mbili na kushindwa mara moja.
Odhiambo ana imani kwamba watakusanya pointi tatu zaidi kwenye mechi yao dhidi ya Talanta ambayo inaongozwa na kocha wa kike Jackline Juma.
"Tumefanya vyema kufikia sasa na sioni chochote kinachoweza kutuzuia kushinda mchezo wa Jumamosi dhidi ya Talanta," Odhiambo alisema.
"Lengo letu ni kushinda mechi nyingi iwezekanavyo na kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu," aliongeza.
Kariobangi Sharks watakuwa wenyeji wa Police FC katika mechi ingine ya Raundi ya 9 ya KPL iliyopangwa kuchezwa Ijumaa ugani Dandora.
Siku ya Jumamosi, Kakamega Homeboyz itakuwa mwenyeji wa Bandari katika Uga wa Mumias Sports Complex huku Muranga Seal wakichuana na Shabana pale St. Sebastian Park.
Nairobi City Stars watatoana kijasho chebamba na Tusker katika uga wa Kenyatta, Machakos.
Posta Rangers watakuwa wenyeji wa Mathare United huku Mara Sugar ikimenyana na Sofapaka.
Siku ya Jumapili, Ulinzi Stars wanapeleka vita kwenye mlango wa Bidco United.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!