
Kocha mkuu wa Mathare United John Kamau amesema wanatarajia mechi kali dhidi ya Posta Rangers katika uwanja wa Kenyatta, Machakos siku ya Jumamosi.
Katika mahojiano ya Ijumaa, Kamau aliwataka wachezaji wake kutodharau Posta.
"Posta ni timu nzuri. Wana uzoefu wa kushindana katika ligi hii kwa hivyo tunakaribia mchezo huu tukifahamu vyema changamoto iliyo mbele yetu. Hatuendi katika mechi hii tukiangalia jinsi walivyopangwa kwenye jedwali la ligi," Kamau alisema.
Mtaalamu huyo atakuwa akiiongoza Slum Boys katika pambano gumu na timu ya daraja la juu aliyoifundisha kwa misimu miwili kabla ya kupoteza kibarua chake. Alijiunga na Mathare mwanzoni mwa msimu.
Anaamini wana uwezo wa kuchomoa ushindi mkubwa huku wakipania kusalia kwenye 10 bora.
“Kwa jinsi tulivyofanya mazoezi hadi sasa naamini tupo tayari kwa mechi hiyo, bila shaka kwenye soka kuna wakati utakuwa juu ya mchezo wako na siku nyingine unajikuta unasuasua.
"Kwa sasa timu yetu iko vizuri na tupo tayari kutumia vyema fomu yetu ili kusajili matokeo mazuri, wachezaji wamejiandaa kiakili, kiufundi na kimbinu na wanaelewa nini kinatakiwa kutoka kwao," alisema.
Ikiwa na pointi 11, Mathare iko katika nafasi ya sita kwenye jedwali na pointi sita nyuma ya viongozi KCB.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!