
Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) umekaribisha uamuzi wa Rais William Ruto wa kufutilia mbali mikataba ya Adani Group.
Katika taarifa siku ya Ijumaa, Katibu Mkuu wa Cotu Francis Atwoli alisema uamuzi huo ulikuwa, hatua ya ujasiri, ya wakati unaofaa na isiyo na shaka.
"Tangazo hili la Rais, lililotolewa Alhamisi wakati wa Hotuba ya pili ya Hali ya Kitaifa Bungeni, limerejesha imani ya wafanyikazi katika sekta zote lakini hasa wale wanaowakilishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga (KAWU) chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya," alisema.
Alibainisha kuwa wanachama wa KAWU wameelezea hofu juu ya masharti ya kandarasi haswa Wahindi kuchukua shughuli za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa zaidi ya miaka 30.
Atwoli alisema kutokana na kughairiwa huko, wafanyikazi wa Kenya wameomba mashauriano nao ipasavyo.
"Tunapenda kukumbusha mashirika yote ya Serikali na Serikali kwamba mashauriano sahihi na wafanyakazi ni lazima kabla ya mageuzi yoyote ya kimkakati," alisema.
Aidha alisema kuwa hatua hiyo ya ujasiri ya Ruto ndiyo dalili ya wazi zaidi kwamba mafanikio ya serikali ya Kenya Kwanza yataondoa mikataba yoyote inayotiliwa shaka na kufanikisha kufunguliwa kwa kesi za ufisadi.
Atwoli alihakikisha kwamba Cotu itaendelea kutoa wito wa kukuza maadili ya mazungumzo ya kijamii kati ya washirika wa pande tatu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!