Kampuni ya Adani ya India siku ya Alhamisi ilipuuzilia mbali mashtaka yaliyotolewa na waendesha mashtaka wa Marekani kwamba mwanzilishi wake Gautam Adani alilipa zaidi ya dola milioni 250 kama hongo ili kupata kandarasi za faida kubwa za serikali.

"Madai yaliyotolewa na Idara ya Sheria ya Marekani na Tume ya Usalama ya Marekani dhidi ya wakurugenzi wa Adani Green hayana msingi na yamekanushwa," Kampuni hiyo ilisema katika taarifa.

Kampuni ya Adani iliongeza kwamba..."njia zote za kisheria zitatafutwa".

Madai hayo yanamtuhumu Adani na wasaidizi wake kadhaa kwa kulipa zaidi ya dola milioni 250 kama hongo kwa maafisa wa India kwa kandarasi za faida kubwa za usambazaji wa nishati ya jua.

Mikataba hiyo ilitarajiwa kutoa faida ya zaidi ya dola bilioni 2 baada ya ushuru kwa takriban miaka 20. Hakuna hata mmoja wa washtakiwa waliotajwa katika kesi hiyo aliye chini ya ulinzi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Tunawahakikishia washikadau wetu, washirika na wafanyakazi kuwa sisi ni shirika linalotii sheria, linalotii sheria zote kikamilifu”, taarifa hiyo ilieleza.