Rais William Ruto amewaongoza Wakenya kwa kumsherehekea mke wake, Mama Rachel Ruto anapoadhimisha siku ya kuzaliwa.

Kupitia kurasa katika mitandao ya kijamii, Ruto alichapisha picha ya pamoja na kumtakia heri njema ya siku yake ya kuzaliwa mama wa taifa.

Kiongozi wa taifa katika ujumbne huo mfupi wenye makopakopa mengi ya mapenzi na mahaba, alikiri kwamba Rachel Ruto si tu Baraka kwake bali pia kwa familia nzima.

Alimaliza kwa kumuombea Baraka tele kutoka kwa Mungu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Heri njema ya siku ya kuzaliwa mpenzi wangu, Mama Rachel Ruto. Endelea kuwa baraka kwangu na kwa watoto wetu. Mungu akubariki sana,” rais William Ruto alisema.

Kwingineko, mama wa taifa, Rachel Ruto alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na watoto katika kaunti ya Nakuru.

Bi Rachel Ruto alijumuika na watoto Nakuru kusherehekea na kuadhimisha siku ya watoto duniani ambayo huadhimishwa Novemba 20 kila mwaka.

Wanandoa wa kwanza wa taifa watasherehekea ukumbusho wao wa miaka 31 wa ndoa mnamo Desemba katika siku ya kuzaliwa ya 58 ya Ruto.