
Kiungo wa Gor Mahia Austin Odhiambo amewaonya wapinzani wao wa jadi AFC Leopards kuwa tayari kwa mechi kali ya Dabi ya Mashemeji.
Vigogo hao wawili wa Ligi Kuu ya Kenya watachuana katika uga wa Nyayo siku ya Jumapili na Odhiambo ameelezea imani kuwa K'Ogalo itaibuka washindi.
"Dabi siku zote ni mchezo mzuri na huu umekuja kwa wakati mwafaka kwa sababu ni fursa kwetu kuwaonyesha mashabiki wetu kuwa tumerejea na kufanya biashara mbaya," Odhiambo alisema.
Mchezaji huyo wa kimataifa vilevile amekiri kwamba alisikitishwa na mashabiki wa klabu hiyo waliozua fujo baada ya klabu hiyo kucheza mechi nne bila ushindi.
Gor sasa inakamata nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Kenya ikiwa na pointi nane. Matokeo hayo mabaya yalisababisha kutimuliwa kwa kocha mkuu Leonardo Neiva.
“Nimesikitishwa sana na jinsi mashabiki walivyoitikia katika mechi mbili zilizopita. Uhuni ni mbaya kwa soka. Kwangu, ilinionyesha kuwa sisi sio familia," Odhiambo alisema.
"Iwapo tunaweza kupoteza mchezo mmoja na mashabiki wakatushambulia inaonyesha hawajali sisi kama wachezaji na wanataka tu tushinde.Ni kawaida sana kupoteza mechi na mashabiki wanatakiwa kusimama nasi katika nyakati nzuri," aliongeza.
Mashabiki walifanya vurugu Jumatano iliyopita Gor Mahia ilipofungwa 2-0 na Bandari mjini Mombasa, wakati wa sare ya 2-2 dhidi ya Murang'a Seal na baada ya kufungwa 2-1 na Nairobi City Stars.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!