Timu ya taifa ya raga


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa Rugby 15, Jerome Paarwater ametaja wachezaji 23 ambao watakuwa nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kombe la Elgon.

Majirani hao wawili wa Afrika Mashariki watamenyana katika mchuano unaotarajiwa kufanyika KingsPark, Bweyogerere siku ya Jumamosi.

Simbas walipiga kambi Kakamega tangu Novemba 10, siku moja baada ya kupata ushindi muhimu wa 27-25 dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa RFUEA.

Mabadiliko pekee yaliyotekelezwa kwenye kikosi hicho ni kutemwa kwa Ernest Obat Kuke ambaye alirejea shuleni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

kocha amemleta Hillary Mwanjilwa kuchukua nafasi ya mchezaji huo huku akiwabeba wachezaji wawili wa ziada Teddy Akala na Beldad Ogeta.

KIKOSI

Ephraim Oduor (Kabras Sugar RFC), Edward Mwaura (Kabras Sugar RFC), Eugene Sifuna (Kabras Sugar RFC), Griffin Musila (KCB RC), Wilhite Mususi (KCB RC), Hillary Mwanjilwa (Kabras Sugar RFC), Ibrahim Ayoo (Menengai Oilers) , Hilary Odhiambo (Kabras Sugar RFC), Griffin Chao (Kabras Sugar RFC), George Nyambua (Kabras Sugar RFC), Jeanson Misoga (Kabras Sugar RFC), Elkeans Musonye (Menengai Oilers), Brian Wahinya (KCB RC), Samson Onsomu (Menengai Oilers), Barry Young (Kabras Sugar RFC), Beldad Ogeta (Menengai Oilers), Andycole Omolo (KCB RC), Walter Okoth (Kabras Sugar RFC), Paul Mutsami (Kenya Harrlequin), Jone Kubu (Kabras Sugar RFC), Emmanuel Silungi (KCB RC), Timothy Omela (Menengai Oilers), Alfred Orege (Kabras Sugar RFC), Teddy Akala(Kabras Sugar RFC), Tyson Maina (KCB RC).

Menejimenti: Jerome Paarwater (Kocha mkuu), Carlos Katywa(Kocha msaidizi), Jimmy Mnene(Meneja), Joseph Guchu (Meneja msaidizi), Steve Mankone (mtaalamu wa fizio), Richard Ochieng (Mkufunzi wa mazoezi ya mwili).