Watu wasiopungua 10 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani kwenye barabara kuu ya Kisumu kwenda Kakamega.

Kulingana na idara ya polisi ajali hiyo ya Jumatano jioni ilitokea katika daraja la Mto Iguhu Yala.

Ajali hiyo ilitokea baada ya lori lililokuwa likisafiri kuelekea Kakamega kupoteza mwelekeo na kugonga matatu iliyokuwa ikielekea eneo la Chavakali mwendo wa saa kumi na mbili jioni.

Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali za karibu zikiwemo za Mbale na Hospitali ya Rufaa ya Kakamega.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans