
Akoth alijumuisha kikosi cha Kenya cha wanawake wasiozidi umri wa miaka 17 kilichowakilisha taifa kwenye Kombe la Dunia katika Jamhuri ya Dominika kuanzia Oktoba 16-Novemba 3.
Ingawa alitimiza ndoto yake ya kucheza katika shindano hilo kubwa zaidi Duniani, Akoth alikumbana na changamoto kubwa aliporejea nyumbani.
Ilimbidi kutafuta usalama baada ya kuambiwa baadhi ya watu walikuwa wakipanga njama ya kumshambulia na kumuibia.
“Niliporudi, nilifahamishwa kuwa watu walikuwa wakipanga kuniibia kwa sababu walidhani nilikuwa na pesa nyingi,” Akoth alisema.
Kwa kuongezea, marafiki zake wote ambao walikuwa wakitembelea nyumba yao kabla ya umaarufu wake, walitoweka ghafla.
"Siwaoni tena marafiki zangu ambao walikuwa wakija kwetu. Wengi wameamua ghafula kujiweka mbali. Watu wananiambia kuwa wananiogopa sasa."
Junior Starlets waliandika historia kwa kuishinda Mexico katika mechi yao ya mwisho lakini wakaondoka kwenye dimba kwa sababu walikuwa tayari wamepoteza mechi mbili za kwanza dhidi ya Uingereza na Korea Kaskazini.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!