
Kiungo wa AFC Leopards Bryan Wanyama akikabiliana na Joseph Okwenda wa Mara Sugar wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya Kenya Uwanja wa Dandora /AFC Leopards
Raia huyo wa Czech alizungumza baada ya mechi yao dhidi ya Mara Sugar kuisha sare kwenye uga wa Dandora siku ya Jumapili. Mshambuliaji wa Mara Sugar, Meshack Karani, alitangulia kufunga dakika ya 43 kabla ya Sydney Lokale kuisawazishia Ingwe dakika za lala salama.
"Nawaomba wachezaji waendelee kufanya kazi kwa bidii. Matokeo mazuri yatakuja hatimaye," Trucha alisema.
Pia ametoa wito wa kuwepo kwa umoja na dhamira. "Safari ya mafanikio haitakuwa rahisi. Tunatakiwa kuwa na nidhamu na umakini katika mchezo wao, pamoja na kusaidiana ndani na nje ya uwanja," aliongeza.
Kocha Mkuu wa Mara Sugar, George Midenyo, alisema alifurahi kupata pointi muhimu ya ugenini, lakini alihisi wangeweza kufanya vizuri zaidi.
"Tulidhibiti mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Tulipaswa kushinda mechi," Midenyo alisema. Midenyo aliwasifu wachezaji wake kwa kuonyesha ukakamavu na ufahamu wa kimbinu.
"Tulijua utakuwa mchezo mgumu, lakini tulikaa makini na kutekeleza mpango wetu kikamilifu. Wachezaji wote wanastahili sifa nyingi kwa juhudi zao nzuri. Safu ya ulinzi ilikuwa imara na kipa wetu alionyesha ujasiri na kutuokoa mara kadhaa,” alisema.
Sare hiyo iliipeleka Mara Sugar hadi nafasi ya pili kwa alama 15, mbili nyuma ya viongozi KCB. Wasagaji sukari wa Narok sasa wana nia ya kuwaondoa wanabenki kutoka kileleni mwa jedwali huku wakipania kunyakua taji lao la kwanza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!