Nahodha wa Shabana FC, George Onyango (kushoto) akichuana na fowadi wa Kenya Police David Simiyu wakati wa mchuano wao wa KPL kwenye uwanja wa Gusii


Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya, Shabana, imemgeukia kocha mzoefu Bernard Mwalala katika harakati za kubadilisha hali yao inayozidi kuzorota.

Timu hiyo yenye maskani yake Kisii ilipata ushindi wa kwanza katika ligi hiyo baada ya kulaza Kenya Police 1-0 katika uwanja wa Gusii mnamo Jumapili.

Kabla ya ushindi huo, Shabana walikuwa wameandikisha sare tatu na kupoteza mechi moja msimu huu. Wiki mbili zimepita tangu Sammy "Pamzo" Omollo ajiuzulu nafasi yake ya ukocha na kuiacha timu hiyo bila mwelekezi.

Klabu hiyo imeorodhesha matokeo duni katika ligi licha ya kutumia pesa nyingi kununua wachezaji wazoefu katika kipindi cha usajili uliopita.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Inasemekana Pamzo alitakiwa kujiuzulu wadhifa wake baada ya msimu kuanza vibaya. Timu hiyo ilimwajiri Peter Okidi wiki mbili zilizopita kukaimu kama kocha mkuu wa muda, huku David Juma, kocha wa makipa, akihudumu kama msaidizi wake.

Mwalala na kiungo wa zamani Osborne Monday waliripotiwa kujumuishwa kwenye benchi la timu hiyo Ijumaa.

Okidi anaonekana kupendekezwa kuchukua nafasi ya ukocha mkuu ikizingatiwa kuwa ni yeye pekee mwenye beji ya CAF A. Mwalala na Monday wote wana leseni B za ukocha za CAF.

Mwalala anarejea katika kiwango cha juu baada ya kuondoka KCB mwezi Juni baada ya kandarasi yake kuisha,  Aliaidia klabu hiyo kutinga fainali ya Kombe la FKF, ambapo walifungwa na Kenya Police.