
Timu hiyo iliyoondoka Nairobi Jumatatu, itamenyana na Zimbabwe Ijumaa kabla ya mechi ya pili dhidi ya Namibia mnamo Novemba 18.
Timu hiyo, iliyoondoka Nairobi Jumatatu, itamenyana na Zimbabwe Ijumaa kabla ya mechi ya pili dhidi ya na Namibia mnamo Novemba 18.
Michezo yote miwili itapigwa kwenye Uwanja Mpya wa Peter Mokaba mjini Polokwane, Afrika Kusini.
Hili linajiri siku kadhaa baada ya mkufunzi mkuu Engine Firat kufichua orodha ya wachezaji 24. Kwa sasa Harambee Stars wako katika nafasi ya tatu katika kundi 'J' baada ya kuzoa alama nne. Cameroon wako kileleni mwa jedwali la kundi hilo wakiwa wamekusanya alama 10 huku Zimbabwe wakijivunia nafasi ya pili na pointi nane.
Kipa mzoefu Patrick Matasi, anayechezea Police FC katika Ligi Kuu ya Kenya, ni mmoja wa wachezaji waliopuuzwa na kocha huyo wa Uturuki.
Mabeki wa Gor Mahia, Sylvester Owino na Geoffrey Ochieng pia wameachwa nje ya kikosi. Wengine ni viungo Alphonce Omija (Gor Mahia) na Chris Erambo (Tusker).
Firat amemjumuisha kikosini mwanasoka mchanga Amos Wanjala, mchezaji wa Nastic nchini Uhispania, ambaye alivutia baada ya kuiongoza St Anthony's Kitale kushinda taji la mashindano ya shule za upili za 2023 akiwa nahodha.
Kikosi
Makipa: Byrne Odhiambo, Faruk Shikhalo, Ian Otieno
Walinzi: Daniel Anyembe, Amos Wanjala, Amos Nondi, Joseph Okumu, Johnstone Omurwa, Charles Momanyi, Eric Ouma, Abud Omar
Wachezaji wa kati: Anthony Akumu, Marvin Nabwire, Duke Abuya, Timothy Ouma, Richard Odada, Austine Odhiambo, Ronney Onyango, Alfred Scriven, Leshan Mootian, Adam Wilson
Washambuliaji: Michael Olunga, Jonah Ayunga, John Avire
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!