Mashemeji wa rais mstaafu Uhuru Muigai Kenyatta wamo katika majonzi.
Familia ya mke wa Uhuru, Margaret Kenyatta, inaomboleza kufuatia kifo cha kaka mdogo wa mke huyo wa rais wa zamani, William Gakuo.
Tangazo la kifo lililofikia Radio Jambo linaonyesha
kwamba marehemu William alipoteza maisha yake mnamo Novemba 6, 2024. Alikuwa na
umri wa miaka 48 wakati alipokata roho.
Marehemu William ni kaka wa aliyekuwa mke wa rais Margaret Kenyatta, Gabriela, Maina, Anna, Christine na Uhuru.
Alikuwa mume wa Sheila Wanjiku Mwangi na alikuwa mjomba wa wengi.
"Marafiki na familia watakuwa wakikutana nyumbani kwa Maina huko Karen Jumamosi 09.11.2024 na Jumapili 10.11.2024 saa kumi jioni," tangazo la mazishi lilisomeka.
Hafla ya maziko ya marehemu itafanyika Jumanne, Novemba 12, mwendo wa saa nne asubuhi.
Kisha mwili wake utachomwa katika eneo la Hindu Crematorium Kariokor baada ya ibada.
Hadi wakati wa kuchapishwa kwa taarifa hii, chanzo cha kifo cha marehemu William kilikuwa bado hakijawekwa wazi.
Marehemu alikuwa ameweka maisha yake kuwa ya faragha sana na maelezo machache sana kumhusu yanapatikana hadharani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!