caption

Wachezaji wa Harambee Stars wakiwa mazoezini

Kocha wa Harambee Stars Engin Firat amefichua orodha ya wachezaji 24 wa timu hiyo kwa mechi mbili muhimu za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 dhidi ya Namibia na Zimbabwe.

Timu hiyo itaondoka Nairobi kuelekea Johannesburg mnamo Novemba 11. Harambee Stars itamenyana na Zimbabwe Jumanne, Novemba 15, na Namibia siku nne baadaye.

Michezo yote miwili itapigwa kwenye Uwanja Mpya wa Peter Mokaba mjini Polokwane, Afrika Kusini.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwa sasa Harambee Stars wako katika nafasi ya tatu katika kundi 'J' baada ya kuzoa alama nne. Cameroon wako kileleni mwa jedwali la kundi hilo wakiwa wamekusanya alama 10 huku Zimbabwe wakijivunia nafasi ya pili na pointi nane.

Kipa mzoefu Patrick Matasi, anayechezea Police FC katika Ligi Kuu ya Kenya, ni mmoja wa wachezaji waliopuuzwa na kocha huyo wa Uturuki.

Beki wa Gor Mahia, Sylvester Owino, pia ameachwa nje ya kikosi. Firat amemjumuisha kikosini mwanasoka mchanga Amos Wanjala, mchezaji wa Nastic nchini Uhispania, ambaye alivutia baada ya kuiongoza St Anthony's Kitale kushinda taji la mashindano ya shule za upili za 2023 akiwa nahodha.

Kikosi

Makipa

Byrne Odhiambo, Faruk Shikhalo, Ian Otieno Walinzi Daniel Anyembe, Amos Wanjala, Amos Nondi, Joseph Okumu, Johnstone Omurwa, Charles Momanyi, Eric Ouma, Abud Omar

Wachezaji wa kati

Anthony Akumu, Marvin Nabwire, Duke Abuya, Timothy Ouma, Richard Odada, Austine Odhiambo, Ronney Onyango, Alfred Scriven, Leshan Mootian, Adam Wilson

Washambuliaji

Michael Olunga, Jonah Ayunga, John Avire