
Siku ya Jumanne, Manchester City ilipoteza mechi yake ya tatu mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2018, baada ya kuchapwa na Sporting Lisbon katika mchuano wao wa nne wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2024.
Vijana wa Pep Guardiola walipokea kichapo cha aibu cha 4-1 huku mshambuliaji Viktor Gyokeres akionyesha umahiri wake wa kufunga mabao kwa kufunga hat-trick kwenye uwanja wa José Alvalade.
Ilikuwa mechi ya kwanza na ushindi kwa kocha Ruben Amorim dhidi ya klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza tangu ateuliwe kuinoa klabu ya Manchester United mwishoni mwa wiki jana.
Mechi ilianza kwa City kupata bao la kwanza dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji Phil Foden. Mabingwa hao watetezi wa EPL hata hivyo hawakuona wavu tena kwa zaidi ya dakika 90 zilizofuata.
Mshambulizi matata wa Sporting Lisbon Viktor Gyokeres alifunga mabao matatu katika dakika ya 33, 49, na 50 huku mwenzake Ronald Araujo pia akiifungia klabu hiyo ya Ureno bao moja.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya kocha Rube Amorim kuteuliwa na klabu ya Manchester United kuchukua mikoba ya Erik ten Hag ambaye alitimuliwa mapema wiki jana kufuatia msururu wa matokeo hafifu.
Mnamo Novemba 1, Klabu ya Manchester United ilitangaza kuzinasa huduma za kocha Mreno, Ruben Amorim. Kupitia taarifa rasmi kwenye tovuti yao,.
Mashetani Wekundu walifichua kwamba Amorim amejiunga nao kwa mtakaba wa hadi 2027 na ataanza majukumu yake rasmi Novemba 11.
“Manchester United inafuraha kutangaza uteuzi wa Ruben Amorim kama Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza cha wanaume, kulingana na mahitaji ya viza ya kazi," United ilitangaza.
“Atajiunga hadi Juni 2027 na chaguo la klabu la mwaka wa ziada, mara tu atakapotimiza wajibu wake kwa klabu yake ya sasa. Atajiunga na Manchester United Jumatatu 11 Novemba.”
Ruben ni mmoja wa makocha wachanga wenye kusisimua na wenye viwango vya juu katika soka la Ulaya.
Akiwa amepambwa sana kama mchezaji na kocha, mataji yake ni pamoja na kushinda Ligi Kuu mara mbili nchini Ureno akiwa na Sporting CP; la kwanza ambalo lilikuwa taji la kwanza la kilabu katika miaka 19.
Ruud van Nistelrooy anaendelea kuinoa timu hiyo hadi Ruben ajiunge nayo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!