Siku ya Jumanne jioni, aliyekuwa mgombea urais wa Kenya na ambaye ni kiongozi wa Thirdway Alliance Party Ekuru Aukot alipiga kura yake katika uchaguzi wa urais wa Marekani.
Katika taarifa yake kwenye mitandao ya kijamii, wakili huyo mashuhuri ambaye kwa sasa anaishi Marekani alifichua kuwa alimpigia kura mgombea urais wa Chama cha Democratic Kamala Harris.
Aukot alionyesha karatasi yake ya kupigia kura ambayo ilithibitisha kwamba hakika alikuwa amempigia kura makamu wa rais huyo wa sasa wa Marekani.
"Nimempigia kura Kamala Harris," Aukot alisema.
Hatua hiyo ilizua hisia mseto kutoka kwa Wakenya huku baadhi yao wakihoji ni vipi ana uraia wa Marekani ilhali anakimezea mate kiti cha urais wa Kenya.
“Kwa
hiyo wewe ni raia wa nchi mbili (Marekani na Kenya) na bado unataka kuwa Rais
nchini Kenya? Tunahitaji kuwa na mjadala huu iwapo utarudi tena,” Mtumiaji wa
mtandao wa kijamii wa X Abraham Mutai alitoa maoni.
Katika majibu yake, Aukot alisema, "Wakati wowote."
Mwaka
wa 2022, kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance aliondolewa kwenye
kinyang'anyiro cha urais wa Kenya kwa kukosa kutia saini ya wafuasi wake kwenye
ukumbi wa Bomas of Kenya.
Aliyekuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati alisema kuwa Aukot pia alishindwa kutoa nakala za vitambulisho vya wafuasi wake.
Aukot alishindwa kutoa saini na nakala za vitambulisho vya kitaifa vya wapiga kura 48,000 waliojiandikisha ambao waliidhinisha azma yake ya urais.
Hapo awali alikuwa amewania kiti hicho cha juu zaidi nchini mwaka wa 2017 lakini akashindwa na Uhuru Kenyatta.
Kwa sasa, kura zinaendelea kuhesabiwa kote Amerika, huku matokeo katika baadhi ya majimbo yakiwa tayari yametangazwa.
Matokeo ya uchaguzi wa Marekani yatangazwa jimbo kwa jimbo,
Je,
matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2024 yanatarajiwa lini?
Kura za kwanza zilifungwa saa 18:00 EST (23:00 GMT) Jumanne jioni. Ya mwisho itafungwa saa 01:00 EST (06:00 GMT) mapema Jumatano.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!