Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee ameandika ujumbe wa faraja kwa watu wote wanaoomboleza baada ya kuwapoteza wapendwa wao mwaka huu.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye
mitandao ya kijamii, msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alisema kuwa kumpoteza
mpendwa si jambo rahisi akibainisha kuwa anaelewa jinsi ilivyo ngumu.
Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba watu kuwa na huruma kwa wengine akibainisha kuwa baadhi ya watu wanaweza kuwa wanaomboleza kimyakimya bila kuonyesha waziwazi.
"Kwa mashabiki wangu wote ambao wamepoteza wapendwa wao mwaka huu, rambirambi zangu za dhati. Kupoteza mtu hadi kifo ni mojawapo ya matukio yenye uchungu zaidi, na ninaelewa uzito wa hasara hiyo,” Akothee alisema kupitia Instagram.
Aliongeza, "Hebu tukumbuke kumtendea kila mtu kwa uangalifu na fadhili, huwezi kujua vita vya kimya ambavyo wanaweza kuwa wakikabili."
Mama huyo wa watoto watano
alifichua kwamba amejifunza kuishi maisha kikamilifu baada ya kushuhudia vifo
vingi vya ghafla mwaka huu.
"Mwaka huu, nimeshuhudia vifo vingi visivyootarajiwa, ukumbusho wa kuthamini maisha kikamilifu. Ishi kwa maana, kwani kifo ni ukweli kwa walio hai,” alisema.
Hivi majuzi, mwimbaji huyo alipoteza shemeji yake David ambaye alifichua kwamba alijitoa uhai katika hali isiyoeleweka.
Katika barua ya kumuomboleza, Akothee alimlilia shemeji yake lakini pia akakosoa uamuzi wake wa kukatisha maisha yake, akiiacha familia yake nyuma.
Msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alibainisha kuwa chaguo la shemejiye limewaacha wengi, wakiwemo watoto wake mwenyewe, wakiwa wamevunjika moyo.
"Jamani shemeji sina nguvu ya kukuhukumu kwa uamuzi ulioufanya wa kuhitimisha safari hii, naomba nikuulize kwanini hukunifikia mimi au hata kwa wapwa zako? lakini labda ulifikiri kila mmoja alinaswa na matatizo yake,” Akothee aliandika Septemba.
"Lakini
sasa, ngoja nikuulize-vipi kuhusu mkeo na watoto wako? Omuga na hao wengine?
Daudi, hukumfikiria mama yako ambaye amekuwa mjane kwa mwaka mmoja tu? Kwa nini
ulikuwa mbinafsi sana, Odebi? Umevunja mioyo ya watoto wangu, "aliongeza.
Mama huyo wa watoto watano pia aliomba msamaha kutoka kwa marehemu, akikiri kuwa wote wameachwa na huzuni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!