
Familia ya masupastaa Marioo na Paula Kajala wamesherehekea binti yao Princess Amarah kutimiza umri wa miezi 6 tangu kuzaliwa.
Wawili hao walichukua sherehe hizo kupitia kurasa zao kwenye mtandao wa picha wa Instagram kumsherehekea mwanao kwa hatua ya kufika umri wa nusu mwaka.
Paula alimwandikia maneno matamu akimtabiri kuwa kichwa na si mkia.
“Heri njema ya miezi 6 ya kuzaliwa malaika wetu, ukawe kichwa na si mkia,’ waliandika kwenye chapisho la pamoja.
Mapema mwezi Mei mwaka huu, Radio Jambo iliripoti kuhsu ujio wa binti wa wapenzi hao wawili ambao penzi lao lilianza kimzaha kabisa.
“Asante Mungu kwa Baraka hii ya Mtoto , tunakushukuru kwa Mtoto wetu wa Kwanza. Binti yetu mrembo @princess__amarah, Mungu Akukuze akujaalie Afya na Baraka Tele ??,” Marioo alisema.
Itakumbukwa penzi lao lilianza baada ya Paula kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, msanii Rayvanny na ukaribu wake na Marioo ulianza wakati alikubali kufanya kazi naye kama vixen kwenye video ya wimbo wake.
Baadae, penzi liliota kati yao na ikabainika kuwa kweli baada ya mamake Paula, Kajala kuhakiki penzi lao na hata kulibariki.
Haikuwachukua muda mrefu kabla ya kutangaza mimba yao na safari ya uzazi ikaanza ambapo walibarikiwa na binti waliyempa jina la ‘Amarah’ Awali, pia tuliweza kukufafanulia maana ya jina hilo na chimbuk lake halisi.
Kwa mujibu wa Mom Junction, Amarah ni jina la kisasa la kike lenye mizizi ya Kiafrika-Amerika, linajitokeza kama kibadala cha kipekee cha Amara. Katika jamii ya Igbo kutoka Magharibi wa Afrika, jina Amarah linaashiria 'neema,'
Huku katika Kisanskrit, moja ya jamii kubwa ya Wahindi, linawakilisha 'asiye kufa' au 'wa milele.'
Asili yake ya Kiarabu inarejelea 'kundi kubwa la meli zinazosafiri pamoja' au 'kabila la kushangaza, Amarah pia jina la mji wa kusini-mashariki mwa Iraqi, na kuongeza utofauti wake.
Ingawa mzizi wa neno Amarah ni lahaja iliyoenea ya Amara, vibadala vingine vya karibu vyenye etimologia tofauti vinaweza kujumuisha Amura, Amare, Amer, Amaro, na Ameerah.
Baadhi ya lakabu za Amarah ni pamoja na Ami, Mara, Arah, Rami, na Hama.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!