Shirikisho la soka la Afrika (CAF) limetangaza kifo cha mwamuzi wa soka wa Ligi Kuu ya Uganda.

Katika taarifa yake mnamo Jumapili, Novemba 3, Rais wa CAF Patrice Motsepe alitangaza kwamba refa Peter Kabugo alipoteza maisha baada ya kuanguka wakati wa mechi.

Marehemu Kabugo alikuwa akisaidia kusimamia mchuano katika uwanja wa Wankulukuku nchini Uganda tukio hilo la kusikitisha lilipotokea.

"Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Dk Patrice Motsepe amesikitishwa sana na kifo cha ghafla cha msimamizi wa mechi ya Ligi Kuu ya Uganda, Peter Kabugo ambaye alianguka wakati wa mechi ya ligi ya kandanda kwenye Uwanja wa Wankulukuku nchini Uganda," Dk Patrice Motsepe alisema katika taarifa yake. .

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Bw Motsepe aliendelea kuwapa pole familia na wadau wa soka wa Uganda na kumtakia marehemu Kabugo mapumziko ya amani.

“Rais wa CAF Dk Motsepe anatoa rambirambi zake na za CAF kwa familia ya Peter Kabugo, Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA) na rais wake Moses Magogo na watu wa Uganda. Roho ya Peter Kabugo ipumzike kwa amani,” alisema.

Marehemu Kabugo alikuwa mwamuzi msaidizi wakati wa mechi kati ya SC Vila na UPDF mnamo Novemba 1, 2024.

Inaripotiwa kuwa alianguka katika dakika ya 73 muda mfupi baada ya Villa kufunga bao la tano, na licha ya jitihada za haraka za kumkimbiza kwenye kituo cha matibabu, alifariki njiani.

Sports Club Villa ilishinda UPDF 5-0, lakini hakukuwa na sherehe baada ya mchuano kukamilika kufuatia kifo cha mwamuzi msaidizi.