Kiungo wa kati wa Fulham, Mnigeria Alex Iwobi amezindua rasmi taaluma yake katika muziki wa rap baada ya kuachia video ya wimbo wake.

Iwobi, ambaye amewahi kuchezea Arsenal aliachia video ya wimbo wake kwa jina ‘What’s Luv’ akionyesha weledi na umahiri wake katika kutema mistari.

Hata hivyo, BBC Sport wanabaini kwamba huu si wimbo wake wa kwanza bali ni wa pili.

Iwobi, ambaye amecheza mechi zaidi ya 260 kwenye ligi kuu, aliweka historia mapema mwaka huu kwa kuwa mwanasoka wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza kuachia wimbo wake wa kwanza, ‘Don’t Shoot’.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Muziki daima umekuwa shauku yangu, na njia yangu ya kujieleza mbali na soka," aliambai BBC Sport.

"Muziki ni chombo kizuri, na siku zote nimekuwa nikiutumia kama njia yenye tija kuelezea jinsi ninavyohisi. Kihistoria hakuna mchezaji yeyote wa Ligi Kuu ambaye ametoa muziki unaohusishwa na jina na sura yake, lakini napenda kuwa tofauti na kufanya tofauti.”

"Nilikulia katika eneo la London ambalo lina changamoto kwa baadhi ya watu, najua jinsi inavyoweza kuwa ngumu na ninashukuru kuwa na jukwaa la kujaribu kuleta mabadiliko. Pamoja na kazi tunayofanya katika jamii, natumai kwamba muziki wangu ni njia nyingine ya kuthibitisha kwamba si lazima vijana wajisikie kuwa lazima watoshee kwenye sanduku moja tu.”

"Nataka wahimizwe kufikia ndoto zao, kuweka umakini wao katika mambo chanya. Kuunda muziki hakuondoi chochote kutoka kwa soka yangu, inanisaidia kuzima."