Klabu ya Manchester United wametangaza kuzinasa huduma za kocha Mreno, Ruben Amorim.

Kupitia taarifa rasmi kwenye tovuti yao, Man Utd walifichua kwamba Amorim amejiunga nao kwa mtakaba wa hadi 2027 na ataanza majukumu yake rasmi Novemba 11.

“Manchester United inafuraha kutangaza uteuzi wa Ruben Amorim kama Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza cha wanaume, kulingana na mahitaji ya viza ya kazi.”

“Atajiunga hadi Juni 2027 na chaguo la klabu la mwaka wa ziada, mara tu atakapotimiza wajibu wake kwa klabu yake ya sasa. Atajiunga na Manchester United Jumatatu 11 Novemba.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ruben ni mmoja wa makocha wachanga wenye kusisimua na wenye viwango vya juu katika soka la Ulaya.

Akiwa amepambwa sana kama mchezaji na kocha, mataji yake ni pamoja na kushinda Ligi Kuu mara mbili nchini Ureno akiwa na Sporting CP; la kwanza ambalo lilikuwa taji la kwanza la kilabu katika miaka 19.

Ruud van Nistelrooy ataendelea kuinoa timu hiyo hadi Ruben ajiunge nayo.

Van Nistelrooy aliongoza Utd katika mechi yake ya kwanza kwenye kipute cha kombe la Carabao dhidi ya Leicester City ambapo walishinda 5-2.

Mholanzi huyo ambaye ameshikilia ukocha kikaimu ataingoza Man Utd Jumapili watakapoikaribisha Chelsea katika uga wa Old Trafford.