October 31, 2024
2 min read
Aliyekuwa
mchekeshaji wa kipindi cha Churchill Show, Mammito Eunice, ameendelea kutoa maelezo
zaidi kuhusu ujauzito wa mtoto wa kwanza aliotangaza mapema wiki hii.
Katika
chapisho siku ya Jumatano, mrembo huyo mcheshi alidokeza kwamba alipata
ujauzito ambao anabeba wakati wa maandamano ya vijana yaliyofanyika nchini
Kenya miezi michache iliyopita.
Mammito
alibainisha kuwa huenda hakuweza kuficha furaha yake baada ya vijana kuvamia
bunge mwezi wa Juni, na hilo likapelekea mimba ambayo anaibeba kwa sasa.
"Maandamano
Baby… Baada ya kuingia bungeni, nadhani nilisherehekea sana!!!," Mammito
alisema chini ya video aliyochapisha Instagram ikionyesha ujauzito wake.
Mchekeshaji
huyo alifichua hayo alipokuwa akitangaza shoo yake ya ucheshi iliyoratibiwa
kufanyika Desemba 20, 2024.
Katika
tangazo lake, alieleza kwamba anahitaji pesa za kumlea mtoto wake ambaye
hajazaliwa.
Enjoying this article?
Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans
"Pata
tikiti zako kwa sababu bish anahitaji pesa za nepi," alisema.
Mammito alitangaza habari za ujauzito wake siku ya Jumanne
katika video ya kibunifu ambayo aliichapisha kwenye mitandao ya kijamii.
Katika video hiyo, mrembo huyo mcheshi alionekana akicheza na
mpira wa kandanda kwenye uwanja usio na watu kabla ya kufichua ujauzito wake
mzito.
“Kwani unataka nishike mipira ngapi? Je, moja haitoshi?"
Mamito alisema baada ya kuonyesha ujauzito wake.
Aliendelea kueleza kuwa ujauzito ni baraka na anaukubali.
“Mimba ni baraka *2. Mimi Mammito, tulipatana na Pappito,
tukatengeneza kapappito,” alisema.
Katika chapisho lingine, Mamitto alitoa shukrani zake za dhati
kwa mashabiki wake wengi ambao walikuwa wamempongeza kwa hatua kubwa ya maisha
ambayo amepiga.
Pia alielezea shauku yake ya kuingia katika uzazi na kukutana
na mtoto wake wa kwanza.
“Asanteni kwa jumbe nzuri za pongezi. Ninashukuru kwa safari
mpya ya #babyto baking,” alisema.
"Moyo wangu umejaa .. siwezi kusubiri kukutana
nawe," aliongeza, akimzungumzia mtoto wake ambaye hajazaliwa.
Mchekeshaji huyo wa zamani wa Churchill Show hata hivyo
hakufichua maelezo zaidi kuhusu ujauzito wake. Mpenzi wake, ambaye pia
anakusudiwa kuwa mzazi mwenzake pia amebaki kuwa kitendawili.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!