Wikendi, seneta wa kuteuliwa Crystal Asige aliweka wazi kwa wafuasi wake kwamba hayuko kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi kwa sasa.

Asige ambaye anawakilisha watu wanaoishi na ulemavu katika seneti, katika taarifa fupi kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii alibainisha kuwa yupo single.

"Kwa ambaye inaweza kuhusu- Ndiyo, niko single," Bi Asige alisema.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha nzuri zilizomuonyesha akiwa amevalia nguo nyeusi.

Mapema mwaka huu, seneta huyo wa kuteuliwa alifichua kwamba alipitia kipindi cha kuvunjwa moyo mwaka jana, 2023.

Katika mahojiano na Dr. Ofweneke mwezi Aprili, alifunguka kuhusu uhusiano wake uliofeli.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alipoulizwa kama amewahi kuvunjwa moyo, Crystal alitabasamu na kusema, "Kuna watu wengi wabaya hapa nje".

Kulingana naye, mpenzi wake wa zamani hakuweza kukabiliana na umaarufu na kung'aa kwake baada ya kuteuliwa kwa nafasi ya useneta.

"Wakati mwingine wanaume wanaogopa wasichana watawaacha wakipata umaarufu na kwa kweli sivyo ilivyo".

Hata hivyo, Crystal alisema kuwa mpenzi wake wa zamani bado huwa anampigia simu licha ya yeye kutopokea simu zake.

"Napendelea kuachana uso kwa uso. Nataka uwe mwanaume wa kutosha na unikabili na unieleze kwanini?"

"Siku hizi siku zote huwa niko kwenye 'blind date'. Inafurahisha kwa sababu bado nahitaji kuona jinsi mtu anavyoonekana kwa sababu napenda aina fulani kwa mwanaume," Cystal aliongeza.

Staa huyo wa nyimbo mwenye sauti nyororo alisema kwamba yeye hutafuta sifa zaidi kuliko mwonekano wa kimwili. 

"Aina yangu ya mwanaume ni mkarimu, mtu ambaye angetaka kuelewa ulimwengu wangu jinsi ninavyoishi, lakini pia mrefu, mweusi na mzuri ni kawaida," alisema